Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limenunua mitambo mitatu ya uchorongaji yenye teknolojia na ya kisasa zaidi kuwahi kutumika hapa nchini. Moja wa mtambo huu  unauwezo wa kuendeshwa kwa kutumia kompyuta na mtu akiwa mbali na mashine.

Tukio hili la uziduzi limefanyika leo tarehe 15 Septemba 2020 kwa kudhihirishia umma wa Tanzania, kuwa Shirika limethubutu na limedhamiria kuleta mapinduzi katika soko la madini kwa kuingia kwa nguvu zote kwenye shughuli za uchorongaji.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mitambo hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila ameipongeza STAMICO kwa hatua kubwa waliofikia na uthubutu wa kuleta ushindani katika soko la uchorongaji amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuleta tija na maendeleo kwa Taifa.

Akiongea kuhusu mitambo hiyo, Mkurugezi wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema ni jambo la kujivunia sana kununua mitambo hiyo ya kisasa.

 “Tumenunua mitambo hii mitatu ya kisasa kabisa na mmoja kati ya huo  mtambo ni Explorac 235  wenye uwezo wa kuchimba hadi mita 500 kwa siku. Mtambo huu ni mpya na  kiteknolojia yake ni ya hali ya juu na hakuna kampuni nyingine ambayo imeshawahi kutumia matambo hapa nchini. STAMICO ndio  shirika la kwanza kuwa na mtambo kama huu.

Dkt. Mwasse ameishukuru Wizara ya Madini kwa maelekezo na ushirikiano unaoendelea kutolewa kwa STAMICO na kutoa rai kwa wadau wadau wa uchorongaji kufanya kazi na STAMICO. Mitambo hii inategemea kusafirishwa Kwenda maeneo mbali mbali tayari kuanza kazi ya uchorogaji mara moja.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: