Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi pamoja na utoaji wa elimu wa wananchi wanaotembelea Banda hilo katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga katika ukaguzi wa viwango wa vitabu vya hesabu katika sekta binafsi na sekta za umma katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. 
Mzee Joseph Temba akisoma moja ya kitabu cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) alipotembelea banda la Bodi hiyo katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. 
Afisa Utafiti kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA), Michael Mwakifuna akimsikiliza Bahati Gewye mara baada ya Afisa wa NBAA kimfafanulia muundo wa mitihani ya Bodi alipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. 
Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, Bertha Kipangula(kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu ufanyaji wa mitihani ya Bodi kwa Koneleth Herzon na Devoth Mateni walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. 
Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu ufanyaji wa mitihani ya Bodi pamoja na ada zinazotolewa na Bodi hiyo kwa wananchi waliotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Magreth Kageya amesema ni kosa kwa baadhi ya Vikundi, Taasisi kuajiri watu na kuwapa vyeo vya Uhasibu na Ukaguzi.

Kageya amesema hairuhusiwi watu kupewa vyeo hivyo bila kupita ngazi maalum katika Bodi hiyo sambamba na kufikia ngazi ya CPA, ameshauri Taasisi, Mashirika hayo kuuliza kwa Bodi hiyo ni mtu wa aina gani anapaswa kuwa Mhasibu au Mkaguzi.

Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema Bodi hiyo kwa sasa ina Kitengo cha (Member Service) ambapo chini yake kuna Audit Quality Review (AQR) ambayo inahusika kukagua kuhakikisha Kaguzi zinafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi na kukidhi viwango vya Kimataifa.

Hata hivyo, Bodi hiyo imeanzisha Mfumo wa usajili kwa Wanafunzi na Wanachama kwa njia ya mtandao, sambamba na usajili wa mitihani ya Bodi na kusajiliwa kwa Wanachama kupitia tovuti ya Bodi hiyo amabyo ni https://www.nbaa-tz.org/.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: