Sunday, 20 September 2020

CCM JIMBO LA SEGEREA KUSHINDA KWA KISHINDONA HERI SHAABAN
CHAMA cha Mapinduzi CCM Jimbo la Segerea wamesema katika uchaguzi wa Mwaka 2020  Chama hicho kitashinda kwa kishindo nafasi zake zote kuanzia ubunge ,udiwani pamoja na nafasi ya Rais .

Hayo yalisemwa na mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi wa kata ya Kiwalani Mussa Kafana ambaye awali alikuwa Chama cha Wananchi CUF, wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Segerea Kata ya Minazi Mirefu , kuomba kura za Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli ,diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Godlisten  Malisa, Pamoja na kura za Rais John Magufuli wote kwa tiketi ya CCM.

Mussa Kafana alisema katika Jimbo la Segerea wakati alipokuwa  UKAWA yeye ndio alikuwa kiongozi amesababisha CCM ikose madiwani Jimbo la Segerea hivyo kwa sasa amerudi CCM  kuunga mkono Juhudi za Rais John Magufuli anagombea udiwani kata ya Kiwalani mbinu zote alizokuwa akitumia UKAWA kupata ushindi atazielekeza CCM waweze kuibuka kidedea.

Alisema  yeye na madiwani wenzake waliokuwa UKAWA kwa sasa wote wapo CCM watashirikiana ili CCM iweze kushika dola Jimbo la Segerea .

Alisema wakati alipokuwa UKAWA yeye alikuwa kiongozi pamoja na madiwani wenzake akiwemo Kassimu Msham wote kutoka CUF  kwa kurudisha maendeleo nyuma katika Baraza la Halmashauri ya Ilala pamoja na Jiji  na toka wamerudi CCM nguvu zote wameziekeza katika chama tawala pamoja na kushirikiana na Serikali  kuleta maendeleo.

Mussa aliwataka wananchi wa kata ya Minazi Mirefu kwa maendeleo nafasi ya ubunge  kumchagua Bonah Ladslaus Kamoli  ,udiwani Godlisten Malisa pamoja na urais John Magufuli.

Alisema Rais John Magufuli amefanya mambo makubwa hivyo lazima juhudi zake ziweze kuungwa mkono katika kuleta maendeleo ya nchi yetu UKAWA alikuwa akipoteza muda  sasa hivi anakula matunda ya CCM.

Kwa upande wake mgombe ubunge wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli alisema katika kata ya Minazi Mirefu na Kiwalani amefanya mambo makubwa katika kuboresha miundombinu ya kisasa ikiwemo Barabara ,Masoko na sekta ya maji katika mradi mkubwa wa Serikali wa UMDP awamu ya kwanza ambao umepita kata hizo ni sehemu ya kujivunia matunda ya Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais John Magufuli ambaye ameiwezesha nchi yetu kufika uchumi wa Kati .

Bonah aliwataka wakazi wa Minazi mirefu wasifanye makosa siku ya Octoba 28 kura zao kwa CCM ngazi ya Rais John Magufuli,Ubunge Bonah Kamoli , pamoja na udiwani Godlisten Malisa ili waweze kuletewa maendeleo haraka.

Bonah alisema atashirikiana na wanachi wake katika kuleta maendeleo kusimamia sekta ya elimu ,sekta ya maji kwa zile kata ambazo bado kupata maji safi na salama pamoja na kuboresha miundo mbinu .

Pia Bonah alisema atawawezesha Wanawake wa Jimbo la Segerea pamoja na vijana na Watu Wenye Ulemavu katika mikopo ya Serikali inayotolewa ngazi ya halmashauri ili waweze kupata fedha wakuze mitaji yao ya biashara waweze kujikwamua kiuchumi .

Naye Mgombea udiwani wa Kata Minazi Mirefu Godlisten Malisa alisema mara baada kuchaguliwa kipaumbele chake  cha kwanza mikakati yeke kujenga Zahanati na Shule ya Msingi ndani ya kata ya Minazi Mirefu.

Alisema atashirikiana na Wananchi wake katika kuleta maendeleo zaidi ndani ya kata hiyo ikiwemo kusimamia miradi ya serikali.

Mwisho
Mkutano wa Jimbo la segerea Kata ya Minazi mirefu
Septemba 19/2020

No comments:

Post a comment