Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano nchini (TCRA CCC) Hilary Tesha akisisitiza jambo leowakati wa mkutano wao na wadau kutoka makundi ya watu wenye mahitaji maalumu Jijini Tanga kulia ni Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma na Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tanga Christopher Kiemi
Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo



 Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tanga Christopher Kiemi akieleza jambo wakati mkutano huo kushoto ni Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma

Katibu wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano nchini (TCRA CCC) Mkoani Tanga Lulu George akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

Sehemu ya wadau wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali kwa umakini


BARAZA la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano nchini (TCRA CCC) limeeleza kwamba huduma ya Pesa Mtandao kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu imepanda kutoka akaunti milioni 17.4 mwaka 2015 hadi kufikia akautini milioni 28 Mei mwaka 2020.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano nchini (TCRA CCC) Hilary Tesha wakati wa mkutano wao na wadau kutoka makundi ya watu wenye mahitaji maalumu Jijini Tanga.

Alisema huo ni utaratibu wao kama baraza kukutana na makundi tofauti tofauti na mpaka sasa wana kamati 12 hapa nchini ambazo wanafanya nao kazi ikiwemo ya mkoa wa Tanga, na mikoa mingine dhumuni likiwa ni kuhakikisha wanawafikia watu wengi kadri ya uwezo wao.

Tesha alisema pia mpaka sasa laini za simu zilizotolewa zimeongezeka kutoka milioni 39 hadi mwezi Machi mwaka huu ni milioni 48.9 kwa sasa huku akieleza kwaamba kuna uwekezano mkubwa zikawa zimeongezeka

 “Lakini pia miamala ya kifedha iliyofanyika kuanzia 2015 hadi Mei mwaka huu imeongezeka kutoka miamala milioni 131.6 hadi milioni 257.4 hiyo inaonyesha namna watu wanavyotumia fedha mtandao ya simu za mkononi kuweka fedha kuanzia desemba 2015 hadi machi 2020”Alisema

 Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma alisema kwamba watu wenye mahitaji maalumu alisema kwenye baraza la ushauri na wasilimia wanataka kuanzia mchakato wa kutunga kanuni maalumu za kuwawaezesha watu wenye ulemavu waweze kupata haki ya kupata habari.

 Alisema kwa mfano kanuni zipo wazi za kulinda watumiaji za mwaka 2018, kanuni za maudhui za Radio na TV mwaka 2018 ambazo zimeboreshwa hivi karibuni mwaka huu na kanuni za maudhui ya mtandaoni iliyoboreshwa zinavipengele kamili vinavyolenga namna gani watoa huduma za mawasiliano waweze kuwahudumia watu walemavu.

Naye kwa upande wake Katibu wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano nchini (TCRA CCC) Mkoani Tanga Lulu George alisema kwamba harakati za kutetea haki za watumiaji zilianza mwaka 1960 huku nchini Marekani.

 

Alisema mwaka 1962 Rais wa Marekani John Kenedy alitangaza rasmi haki nne za watumiaji wa huduma za bidhaa ikiwemo haki ya kupata huduma ya mawasiliano.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: