Mtia Nia wa Jimbo la Hai ambaye Kura zake hazikutosha Martin Munisi kulia akiwa na mtia Nia wa Jimbo la Arumeru magharibi Ezekiel Mollel wakibadilisha mawazo ambapo wagombea wote Hawa walisema japo hawajapita katika kimyanganyiro cha kura za maoni CCM wamejipanga kuwapa ushirikiano wa kutosha wagombea waliopitishwa na Chama chao kupeperusha bendera.

Woinde Shizza ,ARUSHA

MMOJA ya watia wa jimbo la Arumeru Magharibi, Ezekiel Elphas Mollel amejitosa kumuunga mkono mgombea mteule wa CCM, Noar Lembriss Mollel akidai ni operesheni kabambe ya kulikomboa jimbo hilo lililopo chini ya upinzani na kulirejesha CCM ambapo amewaomba wana CCM pia kuwa wamoja katika kumwombea kura Rais John Magufuli na kuacha makundi

Akiongea na vyombo vya habari Ezekiel ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliokuwa watiania 61 wa jimbo hilo amekipongeza chama cha mapinduzi kwa kumteua Noar Lembris akidai kwamba uamuzi huo unapaswa kuzingatiwa na wanaccm kwani zamu yake bado na kuwataka kumuunga mkono mgombea huyo.

Ezekiel amekuwa kada wakwanza kujitokeza hadharani kumuunga mkono mteuli huyo Lembris Noar ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha kupitia Chama cha Chadema kabla hajahamia CCM, akidai kuwa nia yake ya dhati ni kuona jimbo la Arumeru masharibi linatoka upinzani .

Ezekiel ambaye kitaaluma ni Mwalimu,alisema yupo tayari kusubiri wakati mwingine wa kuwania nafasi ya ubunge ila kwa sasa itoshe kusema kwamba nguvu yao ni kukomboa jimbo la Arumeru Magharibi

Aliwataka Wana CCM kuacha makundi na kuungana ,kuwa na umoja ili kukiwezesha chama Cha mapinduzi kupita kwa kishindo.


"Nimesikia Kuna watu wameanza makundi kutokana na matokeo yaliotokea nachotaka kusema kiongozi analetwa na mungu Kama nafasi yako imefika utapita tu Sasa Basi kinachotakiwa sisi Kama Wana CCM tumuunge mkono kiongozi yeyote yule aluependekezwa na chama ili chama chetu kiweze kupata ushindi ,tupate ushindi kwa mafiga matatu Rais ,Ubunge na madiwani"alibainisha Ezekiel

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Chadema chini ya mbunge aliyemaliza muda wake Gibson Ole Meseiyeki ambaye amepata tena uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chadema .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: