Na John Walter-Babati
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara imemfuta machozi Mwalimu mkuu mstaafu wa shule ya Sekondari Galapo katika wilaya ya Babati aliedhulumiwa haki yake kwa kutozwa riba ya asilimia mia tatu na kulazimika kulipa milioni arobaini na mbili baada ya kukopa milioni kumi na nne .
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu,imeeleza kuwa wakati Mstaafu huyo akisubiri mafao yake alikopa kutoka kwa wakopeshaji wa mitaani jumla ya shilingi milioni 14 na alitakiwa kurejesha mkopo wote pamoja na riba mara baada ya kupokea mafao yake ambayo ni asilimia 41 lakini wakopeshaji hao walimlaghai akalipa asilimia 300.
Makungu ameeleza kuwa kutoka kwenye mkopo wa shilingi milioni 14 walaghai hao walijipatia shilingi milioni 42 ambapo kati ya fedha hizo wamefanikiwa kumrejeshea mwalimu huyo shilingi Milioni 20.
Hata hivyo mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara ametoa wito kwa wastaafu wenye shida ya mikopo waachane na mikopo umiza mitaani na badala yake waende benki ya posta ambapo matawi yake yameenea nchi nzima na benki zingine zinazokubali kutoa mikopo kwa wastaafu.
Amesema hilo likizingatiwa tatizo hilo la mikopo umiza haliwezi kuwepo tena hivyo kuisaidia Takukuru kuendelea na majukumu mengine kama yalivyoanishwa na sharia ya kuzuia na kupambana na Rushwa namaba 11/2007.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu msataafu Loth Isaac Ndaalu ameangua kilio kwa furaha mara  baada ya kurejeshewa kiasi hicho cha fedha na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara zinazotokana na mikopo kandamizi  ambapo alitozwa riba ya asilimia kubwa na kulazimika kulipa Zaidi ya makubaliano.
Mwalimu huyo mstaafu ameishukuru Takukuru na serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha kurudisha fedha hizo ambazo alishazipoteza.
Mwalimu huyo mstaafu ameishukuru takukuru na serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha kurudisha fedha hizo ambazo alishazipoteza.
Katika hatua nyingine Makungu amesema katika kipindi cha mwezi april mpaka june mwaka huu, Takukuru mkoani Manyara imefanikiwa kuokoa Milioni 147,897,612.00 ambazo ziirejeshwa kutoka mikononi mwa watu wasiokuwa waaminifu huku sehemu kubwa ya fedha hizo zikiwa ni za mikopo toka katika benki ya Kilimo Tanzania (TADB) .
Aidha kwa upande wa uchunguzi wan a mshtaka,katika kipindi cha kuanzia april jadi juni 2020, TAKUKURU ilipokea jumla ya malalamiko 1305 ambapo kati ya malalamiko hayo, 104 yalihusiana na makosa ya rushwa na malalamiko 31 yalihusu makosa mengine ambapo walalmikaji walishauriwa na kuelekezwa katika ofisi husika kwa ajili ya utatuzi wa malalmiko yao.
Makungu ameongeza kuwa jumla ya kesi saba zilifunguliwa ambapo kesi nne zilihusu halmashauri na viongozi wa serikali za vijiji, kesi mbili zenye jumla ya washtakiwa wane zilihusu watumishi wa mamlaka ya mapato (TRA) kupokea rushwa, na kesi moja ilihusu mwenyekiti na katibu wa Chama cha Mapinduzi tawi la Maisaka Kati mjini Babati kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Amesema  kesi tano zilitolewa uamuzi ambapo washtakiwa walipatikana na hatia na kupewa adhabu stahiki ikiwemo kesi CC.48/2016 ambapo aliyekuwa mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro alihukumiwa miaka saba gerezani ana ameshaanza kutumikia kifungo tangu Mei 7,2020.



Share To:

Post A Comment: