NA MWANDISHI WETU

MJUMBE wa Halmashauri CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Emmanuel Japhet Kamara amechukua na kurejesha fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge  ndani ya CCM Jimbo la Dodoma Mjini.

Kamara amepiga hodi katika hatua yake hiyo ya kwanza huku akisubiria maamuzi ya chama yatakayofuata.

"Nashukuru nimefanikiwa kurudisha fomu niliyoichukua na kuijaza.
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha nguvu ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini na kunipa kibali cha kuijaza na kuirudisha nikiwa salama na Malaika wake wakinizunguka."Alisema

Kamara alimalizia kuwa kwa sasa hatua iliyobaki ni kuwaomba Wananchi na Wanadodoma kumuombea kwa Mungu azidi kumpa uhai na afya.

Mwisho
Share To:

Post A Comment: