Tumekuwa tunakula tango bila kufahamu faida zake, basi wacha nikwambie kuwa tango linafaida nyingi sana katika miili yetu tunapokula kila siku.

Uwenda unajiuliza je ni faida zipo hizo zinazopatikana katika tango 'ninapokuwa nakula kila siku'.

Basi ondoa shaka MSUMBA BLOG leo tumekuandalia faida 5 tu za ulaji wa tango katika mwili wa binadamu na kiafaya;

1. Tango huupa mwili vitamin kwa asilimia 95, usaidia kuondoa sumu mwilini.


2. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo husaidia kupunguza aina mbalimbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.

3. Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri, kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kamba kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

4. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari.

5. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis).

Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue).

Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).

Faida hizo upatikana kwa kuzingatia ulaji wa tango kila siku.
Share To:

Post A Comment: