Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Afya ya Mimea (Na. 2) wa Mwaka 2020 (The Plan Health Bill, 2020. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote kuwa humu ndani ya Bunge lako Tukufu kwa ajili ya kujadili Muswada huu. Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji kwa maoni na ushauri wao kuhusu Muswada huu ambayo yamezingatiwa kama inavyoonekana katika Jedwali la Marekebisho (Schedule of Amendment)

Vilevile, napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kutoa maoni katika hatua zote za kuandaa Muswada huu.  Napenda, nimshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maoni na ushauri wake uliofanikisha kutungwa kwa Muswada huu. Aidha, kipekee kabisa napenda nimshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo na maelekezo yake yakuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria mpya ya Afya ya Mimea ya Mwaka 2020 kwa kufuta Sheria ya Hifadhi ya Mimea, Sura ya 133 (Plant Protection Act, 1997) na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki, Sura ya 161 (The Tropical Pesticides Research Institute Act, 1979). 

Lengo la Sheria inayopendekezwa ni kuweka mfumo wa pamoja wa kisheria wa usimamizi na udhibiti wa afya ya mimea, mazao ya mimea na viuatilifu. Aidha, ili kuimarisha na kuweka mfumo bora wa utekelezaji wa masharti ya Sheria inayopendekezwa, inapendekezwa kuanzisha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu ambayo itakuwa ndicho chombo cha usimamizi wa afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu. 

2. LENGO LA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, lengo la Muswada huu ni Kutungwa kwa Sheria ya Afya ya Mimea ya Mwaka 2020.

3. MADHUMUNI YA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, Muswada huu unapendekeza kutungwa kwSheria ya Afya ya Mimea ya mwaka 2020. Lengo la Sheria inayopendekezwa ni kuunganisha Sheria ya Hifadhi ya Mimea, Sura 133 na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifvya Kitropiki (TPRI), Sura 161, ili kuondoa upungufu katika mfumo wa sasa wa kisheria na muingiliano baina ya Sheria hizo zinazopendekezwa kufutwa. Hatua hii itasaidia kuimarisha mfumo utakaosaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za uingizwaji na usambazaji wa viuatilifu bandia.

Mheshimiwa Spika Vilevile Tanzania imeridhia Itifaki na Mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa inayosimamia afya ya mimea na matumizi ya viuatilifu kwenye kilimo kwa lengo la kukidhi matakwa ya masoko.

Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi ya Mimea (International Plant Protection Convention – IPPC) wa mwaka 1997 ambao Tanzania iliridhia tarehe 21 Oktoba, 2005.  Mkataba huo unalenga kuzuia kuingia na kusambaa visumbufu vya karantini vya mimea na mazao katika nchi wanachama kwa kuzingatia matakwa ya kimataifa ya usafi wa mimea. 

Matakwa ya mkataba kwa nchi wanachama ni pamoja na kuwa na chombo mahiri cha kitaifa kinachojitegemea cha kusimamia hifadhi ya mimea yaani “National Plant Protection Organization – NPPO” na kuwa na sheria inayotambua miongozo ya kimataifa ya usafi wa mimea (International Standard for Phytosanitary Measures - ISPMs).

Mheshimiwa Spika, Sambamba na kuanzisha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (NPPO), Muswada huu unapendekeza masharti kuhusu udhibiti wa viuatilifu, usimamizi wa afya ya mimea, udhibiti wa kuzuia kuingia na kuenea kwa visumbufu vya mimea na mazao, udhibiti wa usafi wa mimea, utaratibu wa usimamizi wa majaribio ya ufanisi wa viuatilifu, kuwezesha biashara ya mimea na mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi, pamoja na mambo mengine yanayohusiana na afya ya mimea na viuatilifu kufanyika kwa ufanisi zaidi.

4. MAMBO MUHIMU KATIKA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, baadhi ya mambo muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huu ni pamoja na:-
(a) Kuanzisha Mamlaka itakayosimamia afya ya mimea na viuatilifu;
(b) Kuweka utaratibu wa kusimamia uingizwaji, utengenezaji, usambazaji na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu;
(c) Kuweka utaratibu wa kutambua, kukusanya na kuteketeza au kurudisha viuatilifu bandia, chakavu na vibebeo vilivyokwishatumika;
(d) Kumpa mamlaka Msajili wa Viuatilifu kukasimisha baadhi ya majukumu yake kwa mfanyakazi mwingine wa Mamlaka baada ya kupata ridhaa ya Bodi ya Wakurugenzi;
(e) Kuwezesha Mamlaka itakayoundwa kusimamia masuala ya afya ya mimea na kutoa idhini kwa maabara nyingine kufanya uchambuzi wa ubora wa viuatilifu;
(f) Kuweka viwango vya adhabu kulingana na uzito wa kosa lililotokea;
(g) Kuweka kifungu kinachohusu uchunguzi wa visumbufu (pest surveillance) ili kuwezesha udhibiti wa visumbufu kwa kutumia mbinu sahihi;
(h) Kuipa Mamlaka inayopendekezwa jukumu la kufanya majaribio ya utendaji wa viumbe marafiki, ubora na ufanisi wa viuatilifu (bio-efficacy trial);
(i) Kuweka taratibu au mwongozo wa kukabiliana na visumbufu  vamizi/vigeni;
(j) Kuweka vifungu vya sheria vitakavyoimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali; na
(k) Kuzingatia masuala yote muhimu yaliyokuwepo katika Sheria ya Hifadhi ya Mimea, Sura ya 133 na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kitropiki, Sura ya 161

5. MATOKEO YA SHERIA INAYOPENDEKEZWA KUTUNGWA
Mheshimiwa Spika, Matokeo ya kutungwa kwa Sheria ya Afya ya Mimea ni kama ifuatavyo:
i. Kufutwa kwa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticide Research Institute-TPRI Act) Na. 18 ya mwaka 1979 na Sheria ya Hifadhi ya Mimea (Plant Protection Act- PPA) Na. 13 ya Mwaka, 1997;
ii. Kuondoa vifungu vya sheria vinavyohusu udhibiti wa viuatilifu vya mifugo na afya ya jamii katika Sheria itakayotungwa;
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika shughuli za afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu kutokana na kutumika kikamilifu kwa miundombinu, rasilimali watu na vitendea kazi;
iv. Kuongezeka kwa masoko ya bidhaa za mazao ya kilimo kutokana na kukidhi matakwa ya viwango vya ubora vya afya ya mimea na usafi wa mazao ya kilimo;
v. Kupungua kwa taarifa za malalamiko ya kutokidhi vigezo vya masoko (non-compliance notifications) kutokana na kuimarika kwa udhibiti na ukaguzi wa mazao na viuatilifu;
vi. Kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya kilimo na biashara ya mazao kutokana na kupungua kwa urasimu wa upatikanaji wa huduma za afya ya mimea na viuatilifu;
vii. Kuongezeka kwa uhakika wa chakula na lishe na malighafi ya viwanda kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo;
viii. Kupungua kwa madhara ya kiafya kwa binadamu yatokanayo na masalia ya viuatilifu, sumukuvu, madinizito (heavy metals) na visibika (contaminants) kwenye mazao kutokana na kuimarika kwa mfumo wa udhibiti;
ix. Kupungua kwa viuatilifu bandia/feki sokoni kutokana na kuimarika kwa udhibiti wa viuatilifu katika utengenezaji, uingizaji, usambazaji na uuzaji;
x. Kupungua kwa uvamizi wa visumbufu vipya/vigeni kutokana na kuimarika kwa huduma ya uchunguzi wa visumbufu (pest surveillance);
xi. Kupungua kwa upotevu wa mazao kabla na baada ya kuvuna kutokana na kuimarishwa kwa huduma za udhibiti wa visumbufu;
xii. Kupungua kwa athari hasi kwa mazingira na viumbe vingine zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu, mrundikano wa viuatilifu chakavu na vibebeo vilivyokwisha tumika (obsolete pesticides and pesticides empty containers);
xiii. Kuondoa jukumu la utafiti wa msingi lililokuwepo kwenye Sheria ya TPRI ambalo litafanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo –(TARI) yenye jukumu hilo kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Na. 10 ya Mwaka 2016;
xiv. Kuongezeka kwa maduhuli ya Serikali na;
xv. Kupungua kwa matukio ya ukiukwaji wa sheria kutokana na adhabu zitakazowekwa kulingana na uzito wa kosa.

6. MPANGILIO WA MUSWADA
Mheshimiwa Spika, Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Kumi (10)
Sehemu yKwanza, inahusu masharti ya utangulizi ambayyanajumuisha jina la Muswada, tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria, matumizi na tafsiri ya maneno na misemo mbalimbali iliyotumika katika Muswada pendekezwa.
Sehemu ya Pili, ya Muswada inahusu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu ambayo ndio itakuwa na jukumu la kusimamia uhifadhi wa afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu. Sehemu hii inaainisha pia mamlaka na majukumu ya Mamlaka hiyo.
Sehemu ya Tatu, inajumuisha masharti ya utawala wa MamlakaSehemu hii inaelezea uanzishaji na majukumu ya Bodi, muundo wake, umuhimu wa kuzingatia usawa na masuala yanayohusu mgongano wa masla

Share To:

Post A Comment: