Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ameonyesha kukasirishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani kazi inayofanywa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Jafo ameonyesha hali hiyo Kutokana na kusuasua kwa ujenzi huo zaidi ya miaka miwili hadi sasa Waziri Jafo ameelekeza TBA kumaliza awamu ya kwanza ya ujenzi huo ifikapo Mei 30,2020 kisha halmashauri itafute wajenzi wengine wa kumalizia jengo hilo.

Wakati huo huo Waziri huyo alifanikiwa kukagua ujenzi wa jengo la halmashauri ya Kibaha Vijijini pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya halmashauri hiyo.

Jafo amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kuacha kufanyakazi kwa mazoea na amewaagiza watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia miradi ipasavyo.

Katika ziara hiyo Jafo amewapongeza mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamood Abuu Juma kwa kuwapambania wananchi wao katika kuwaletea maendeleo.



Share To:

Post A Comment: