MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amewataka walimiki wa vyombo vya usafiri wa umma hususani daladala kuangalia upya kiasi cha fedha wanachokihitaji kukusanya kila siku kutoka kwa madereva wao kufuatia janga hili la Ugonjwa wa Covid-19.mwandishi Esther Macha anaripoti toka Mbeya 

Chalamila alitoa kauli hiyo, mwishoni mwa wiki wakati akiongea na madereva wa daladala  wa vituo vya Kabwe na Mwanjelwa na Stendi kuu vilivyopo jijini Mbeya.

Alisema kutokana na janga hilo  na kutolewa miongozo mbalimbali katika kukabiliana nalo ikiwemo abiria kukaa wote kwenye siti na kupunguza msongamano imechangia malengo ya wamiliki wa daladala kutotimia ukilinganisha na ilivyokuwa awali kabla ya ugonjwa kuingia nchini.

“Wamiliki wote wa vyombo vya usafiri wa umma hususani daladala kipindi hiki mnapaswa kuwa waungwana kwa sababu kwa hali iliyopo haruruhusu abiria kujazana kwenye magari ili kujikinga na maambukizi, msipende sana hela kuliko uhai wa watanzania wenzetu shusheni viwango vilivyowapimia madereva wenu,” alisema Chalamila.

Aliongeza kuwa  madereva wa daladala wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuwa wanahatarisha kazi zao kutokana na kushindwa kutimiza malengo yao na mabosi wao wamekuwa wagumu kuelewa wakihisi wanaibiwa.

Miongoni mwa madereva hao, Justin Shaban alieleza kuwa tangu kutolewe marufuku ya kujaza abiri ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona hali ya kiuchumi imekuwa mbaya.

Alisema awali alikuwa akipeleka malengo kwa bosi kwa siku  shilingi 6000 kwa sababu gari yake ni Kosta lakini kwa waendasha haisi ni shilingi 40000.

Shaban alisema kwa sasa wanapeleka malengo kuanzia shilingi 30000 hadi 20000 kwa madai abiria wamepungua lakini pia katazo la kutojaza abiria pia lichangia
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: