Mkuu wa wilaya ya Monduli Mheshimiwa Iddi Kimanta ameipongeza idara ya Elimu Msingi kwa kuanzisha mkakati kupambana na ugonjwa wa maambukizi ya homa ya mapafu Corona #COVID-19 katika shule zote za msingi wilayani humo.

Ametoa pongezi hizo wakati wa kuzindua mpango huo leo ofisini kwake katika hafla ambayo ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli Ndg.Stephen Ulaya, Afisa Elimu Msingi wa Wilaya Ndg.Theresia Kyara, Maafisa Elimu kaitka Idaya ya Elimu, na Maafisa Elimu wa Kata.

Kwa upande wake Ndg.Theresia Kyara ambaye ni Afisa Elimu Msingi Wilaya ameelezaa kuwa, "Kama Idara ya Elimu Msingi tunaunga mkono jitihada za serikali kupambana na Ugonjwa wa COVID_19 unaosababishwa virusi vya Corona.Tuna mkakati wa awamu tatu;

Awamu ya kwanza nikutoa Vifaa kwa walimu katika ofisi zote za shule ya msingi, ambapo Maafisa Elimu, Maafisa Elimu wa Kata na Walimu Wakuu wote wamechanga fedha ambazo zimewezesha kununua ndoo na sabuni tiririka chupa 300 zitazotumiwa na Ofisi za Walimu Wote Wilayani Monduli.

Awamu ya pili tutatoa Elimu kwa walimu wa afya na wanasihi ili shule zikifunguliwa kila asubuhi watoe Elimu kwa wanafunzi.

Awamu ya tatu, Tutaifanya tukishirikiana na wadau wa Elimu wakiwemo wazazi kuhakikisha wanafunzi wote shule za msingi wanapata Barakoa, ndoo, sabuni na maeneo ambayo yanachangamoto za maji watapata vitakasa mikono.
Tumeona ni vyema tujipange mapema shule zikifunguliwa waanze masomo.

Share To:

Post A Comment: