Na Woinde Shizza ,ARUSHA

Watu wawili wamefariki Dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo katika wilaya ya Arumeru huku nyumba zaidi ya 50 kuharibika kutokana na mvua hizo  

Akitoa Taarifa za hali ya mwendendo wa mvua hizo mara baada ya kufanya ziara na kushiriki shughuli za uokoaji, Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jery Muro alisema kuwa mvua hizo  zimeleta madhara makubwa kwani zimesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefariki leo Alhamisi   April 23 Katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha.

Muro aliwataja waliofariki dunia kutokana na mvua hizo  kuwa ni  Terevaeli mirisho Nasari Mwenye umri wa  miaka 65 Mkazi wa kitongoji cha meto kijiji cha mulala kata ya songoro, ambapo amefariki Dunia Asubuhi baada ya maporomoko ya Udongo kutoka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kufariki Dunia papo hapo, na tayari mwili wake umepatikana na kupelekwa katika hospital ya Mount Meru.

Aidha alimtaja kifo  kingine  ni cha mtoto alietambuliwa kwa majina ya  Tumaini Simon Mwenye umri wa miaka 3 Mwenyeji wa kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambae amesombwa na mafuriko ya maji wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na Mzazi wake ambapo Mzee simon alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja na mwingine kufariki dunia na mwili wa mtoto tumaini umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.

Alibainisha Katika Mvua hizo  Nyumba zaidi 50 zimeharibiwa uku zingine zikianguka kutokana na maji kuwa mengi na tayari huku aliongeza 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: