MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepokea magari mawili kutoka kwenye shirika la Afya Tanzania (PSI)ambayo yatakayo saidia kufanya shughuli za kupambana na ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.anaripoti mwandishi Amon Mtega kutoka Songea 

Mndeme akipokea msaada wa Gari hizo  amesema kuwa yatafanya  kazi mkoani humo dhidi ya kupambana na ugonjwa wa Covid 19 ambao umekuwa tishio   Duniani.

Amesema kuwa gari hizo zimeongeza nguvu katika suala nzima la kupambana na ugonjwa huo ambapo yatatumika kwenda kwenye maeneo yanayokuwa na uhitaji ikiwemo kwenye eneo la Mkenda lililopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

   Amefafanua kuwa msaada huo umefika kwa wakati muafaka katika kipindi hiki, ambapo gari moja limeenda Mkenda kwenda kuwachukua watu 13 ambao ni watanzania waliotokea Nchi ya Msumbiji kuwa watawekwa kwenye uangalizi  kwa siku 14(Cratine).

Kwa upande wake  wa PIS kanda za nyanda za juu kusini Edgar Mchaki amesema kuwa magari hayo wameyatoa ili kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya mapambano na ugonjwa wa Covid 19 ,hadi pale utakapokuwa umeisha.

Mchaki amesema kuwa wametoa magari hayo pamoja na madereva ambao watakuwa wanalipwa na shirika hilo katika kipindi chote cha mapambano ya kuzuia ugonjwa huo.

                              

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: