Thursday, 23 April 2020

Mkuu wa wilaya ya Monduli aridhishwa na ujenzi wa nyumba za walimu Ole Sokoine
Na John Walter- Monduli
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta  ameitembelea shule ya Sekondari Ole Sokoine  iliopo kata ya Monduli juu na kukagua hatua za ujenzi wa nyumba mbili za walimu

Gharama  za ujenzi wa nyumba hizo inatajwa kuwa shilingi milioni  mia moja (100) huku wananchi wa Kata za Monduli juu na Mfereji ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo wakiunga mkono hatua hizo ya ujenzi  kwa kufanya kazi za mikono kwa  kuchimba msingi,kukusanya mawe pamoja na kuchimba mashimo ya vyoo ili  walimu waweze kuwa karibu na shule na kuwafanya wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao.

Aidha  Kimanta amewapongeza  wananchi hao kwa kuunga mkono jitihada hizo za mandeleo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya Iddi Kimanta aliongozana na  Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Stephine Ulaya na Mhandishi wa wilaya Eng. Peter Shemahonge.

No comments:

Post a comment