Na Said Mwishehe, 

MKUU  wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo amesema wataendelea kuchukua hatua ya kuchapa viboko watu ambao watakuwa wanafanya mikusanyiko ambao haitakuwa wa lazima hasa kwenye Baa huku akisisitiza watu watachapwa kweli kweli.

Chongolo amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog wakati anafafanua msimamo wa kuchukua hatua ya kuwacharaza viboko watu ambao watakuwa wanaweka mkusanyiko usio wa lazima wakati Serikali inachukua hatua ya kukabiliana na Covid-19.

Amesema " Ufafanuzi Ni rahisi kweli hatuwezi kulea watu wapuuzi ambao wanakiuka utaratibu, Serikali imesema ni marufuku kufanya mikusanyiko isiyolazima, baa sio mkusanyiko wa lazima ,hatuwezi kulea watu ambao wanajitengenezea mikusanyiko ya kupata maambukizi ya Corona.

"Halafu wakishapata mzigo unabaki kuwa Serikali, katika hili hatuwezi kukubali na hatua mchezo na tutachukua hatua kwa yoyote ambaye tutamkuta amejitengenezea mkusanyiko usio wa lazima,"amesema Chongolo.

Amehoji  hivi watu wamelogwa, kwani hawawezi kuchukua kinywaji na kwenda kunywea nyumbani na kwamba Serikali inahangaika kutoa elimu lakini watu bado wanakaidi na kujaa baa." Wakipata maambukizi ya Corona mzigo unabaki kuwa Serikali, mimi nimeagiza wachapwe viboko kweli kweli na ujumbe utakuwa umefika.

"Siku mbili hizi tumewachapa viboko kweli kweli ,hatutafanya mchezo kwenye hilo,tukikuta mkusanyiko usio na sababu za msingi sisi ni fimbo kwa kwenda mbele.Nasema hivi hatua ya awali kwanza ni viboko.

"Kuna watu jana wamekipata kile walichokuwa wanakitafuta,waende mahakamani kunishtaki,lakini kwa sasa tutakuwa tumewasadia kuepukana na Corona."
Share To:

msumbanews

Post A Comment: