Watenda kazi wa taasisi ya Yes-Tz wakiwa katika kikao mkakati cha kujipangia kufanya kazi kwa kinga dhidi ya Corona 
Mkurugenzi wa taasisi ya Yes -Tz Keneth Simbaya akiwa kwenye kikao hicho  picha na habari na Esther Macha, Mbeya

MKURUGENZI wa Shirika lisilo kuwa la kiserikali linalotoa elimu kwa vijana kupitia michezo  (YEs-Tz)Kenneth Simbaya amewataka waandishi wa habari nchini kutoa taarifa sahihi  na kusahihisha habari zinazopotoshwa juu ya homa ya ugonjwa wa Corona .

Simbaya amesema hayo wakati akizungumza na mtandao huu juu ya uvumi ambao umekuwa ukisambaa juu ya homa ya ugonjwa wa homa ya Corona.

Alisema kuwa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kutoa habari za ukweli kuhusiana na homa ya ugonjwa wa corona maana uvumi ni mwingi sana unaosambaa kuliko ukweli.

Hata hivyo Mkurugenzi hutyo alisema kwamba katika kipindi hiki ni vema waandishi wa habari wakaanza kusahihisha upotoshwaji unaotolewa na watu na kuandika habari zenye usahihi kupitia wizara ya afya na shirika la afya duniani .

"sababu haya mambo kuna watu wake wa kuyasemea ambao wana kuwa na vyanzo sahihi lakini si upotoshaji "alisema Simbaya.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema wananchi kupiga simu kwa wataalamu wa afya pale wanapoona dalili za ugonjwa huo ni vema kufika kutibiwa hospitali.

Alisema kuwa Shirika hilo pia limeunga juhudi  za serikali za kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ambapo wameanza kufanya kazi ya kutoa elimu kwa vijana kupitia mitandao ya kijamii badala ya njia ya awali ambayo walizoea kufanya ili kuweza kupambana na homa ya ugonjwa wa corona ambayo iliingia march 15 mwaka .

Alisema kufuatia uwepo wa ugonjwa kunaweza kuwepo unyapaa hivyo waabndishi wa waandishi wa habari  bado wana jukumu kubwa  la kutoa elimu kupitia kalamu zao.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika hilo ,Navina Mutabazi alisema kuwa bado elimu inaendelea kuwafikia vijana  kwa njia mbali mbali  ikiwemo kupiga simu kwa kushirikiana na wataalam wa afya kwa kutumia mitandao ya kijamii .


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: