Monday, 16 March 2020

Waziri Kairuki Agawa Taulo za Kike kwa Wanafunzi SameNa Ferdinand Shayo,Killimanjaro.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angellah  Kairuki amegawa msaada wa taulo za kike kwa  wanafunzi wa shule ya sekondari Makanye  iliyoko wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro lengo ikiwa ni kuwasaidia watoto wa kike wanaotoka kwenye kaya zenye uhitaji waweze kupata msaada huo.

Akikabidhi taulo hizo ,Kairuki amepongeza juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote bila kubagua jambo ambalo litawawezesha watoto wa kitanzania kutimiza ndoto zao.

Kairuki amewataka watoto wa kike kujiepusha na vishawishi na mahusiano kabla wa wakati muafaka ili wasikatishe ndoto zao kwa mimba za utotoni.

“Hapa kuna madaktari,mawaziri,wakandarasi hivyo tunaomba msome kwa bidii ili muweze kutimiza malengo yenu” Alisema Kairuki

No comments:

Post a comment