Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Jumanne Machi 10,2020 Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Jumla ya Vijana 141 kutoka wilaya ya Shinyanga wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Jumanne Machi 10,2020 Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Jumla ya Vijana 141 kutoka wilaya ya Shinyanga wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019.
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta akizungumza wakati hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Jumanne Machi 10,2020 Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Jumla ya Vijana 141 kutoka wilaya ya Shinyanga wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipokea Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiongozana na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege kukagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akielekea kuketi baada ya kukagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amekaa na  Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali Justas Kitta (wa pili kushoto) na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 82 Old Shinyanga,  Meja Saleh Ally na Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 516 Kizumbi, Meja Benard Emmanuel kwenye Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akiwa kwenye hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) na Viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa wa haraka mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakionesha mchezo wa  singe.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakicheza kwaito.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akimkabidhi Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Sajenti Geofrey Kamala zawadi ya fedha kwa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliotoa burudani kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Ili kufanikisha hafla hiyo, Kampuni ya Jambo pia ilichangia vinywaji baridi vyenye thamani ya Shilingi 300,000/=. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jumla ya Vijana 141 wa wilaya ya Shinyanga Wamehitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyodumu kwa kipindi cha miezi kuanzia Novemba 4,2019 hadi Machi 10,2020.
Hafla ya Kufunga Mafunzo hayo imefanyika leo Jumanne Machi 10,2020 katika Viwanja vya Sabasaba katika kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya hiyo,amewataka wahitimu wa mafunzo kuonesha kwa vitendo uadilifu, uaminifu na uzalendo wao katika nchi.
Mboneko aliwataka askari hao ambao wanafanya kazi kwenye Makampuni mbalimbali kutojihusisha na vitendo vya uhalifu badala yake wawe mfano bora kuimarisha ulinzi katika jamii.
“Baada ya kumaliza mafunzo haya nina imani mtakwenda kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha vitendo viovu vinaisha kwenye maeneo yenu. Shirikianeni na Jeshi la polisi kuwabaini wahalifu na msaidie katika kuimarisha ulinzi katika jamii”,alisema Mboneko.
Mkuu huyo wa wilaya aliyaagiza Makampuni yote ya Ulinzi katika wilaya ya Shinyanga kuhakikisha yanakuwa na sare aina moja akieleza kuwa baadhi ya Makampuni ya Ulinzi yamekuwa na sare zaidi ya tatu.
“Nataka kila Kampuni ya Ulinzi itumie Walinzi waliopitia Mafunzo ya Jeshi la Akiba na kila Kampuni iwe na sare moja na ihakikishe inawapa mikataba ya ajira walinzi wake na kuwapatia mishahara kwa wakati”,alisema Mboneko.
Mboneko alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawaruhusu watoto wao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Akiba.
Aidha aliyashukuru Makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd iliyochangia vinywaji baridi ‘soda na maji’ vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 300,000/= kufanikisha mafunzo hayo ya Jeshi la Akiba.
Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga,Kanali Justas Kitta aliwataka Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba kuzingatia nidhamu,kuwa waaminifu na watiifu pamoja na kuwa nadhifu.
“Sitegemei kuona mhitimu anakamatwa na polisi kwa makosa mbalimbali,kuweni watiifu kwenye maeneo mliyoajiriwa na muwe wasafi”,alisema Kanali Kitta.
Akisoma Risala ya wahitimu, Recho Membo alisema walianza mafunzo hayo wakiwa 198 lakini waliofanikiwa kumaliza mafunzo hayo ni 141 kati yao wanaume ni 101 na wanawake 40.
Share To:

Post A Comment: