Wednesday, 11 March 2020

MBUNGE MTULIA AMEZIAGIZA HALMASHAURI KUNUNUA MAFUTA YA ALBINONA HERI SHAABAN
MBUNGE wa Kinondoni Mohamed Mtulia ameziagiza halmashauri nchini kutenga bajeti kwa ajili ya kununua mafuta ya albinism.

Mbunge Mtulia aliyasema hayo jana wakati wa matembezi ya hisani ya kuchangia fedha za mafuta ya ngozi ya Albinism matembezi hayo ya hisani yaliandaliwa na TCA kwa kushirikiana na TAS ,FAT na FEZA.

"Albinism ni wezetu halmashauri wanapotenga fedha za ununuzi wa dawa waweke fungu la kununua matuta ya ngozi ya jamii ya Albinism "alisema Mtulia

Katika hatua nyingine ameagiza  MSD kuweka mafuta ya albinism wasikiuke agizo la serikali halmashauri zinapofuata dawa waweke mafuta hayo.

Alisema katika manispaa ya Kinondoni wapo jumla ya Albinism 320 na mafuta yakifika kila kituo cha Afya yatapelekwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Vipodozi Tanzania Shekha Nasser alisema chama cha Vipodozi Tanzania kimezinduliwa mwaka jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Ummy Mwalimu.

Shekha alipendekeza viwanda nchini kutengeneza mafuta ya ngozi ya watu wenye ulemavu 
Albinism.

Alisema Tasinia ya ya urembo Tanzania imejikita katika masuala mbalimbali ya afya ya urembo hapa nchini kwa kutengeneza bidhaa bora zenye viwango.

Naye Mwenyekiti wa Feza Alumni Fondation Hamza Salehe alisema dhumuni la matembezi hayo kwa ajili ya kununua mafuta ya ngozi ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kofia ngumu.

Hamza alisema chama cha Watu wenye ulemavu, wadau wameweza kufanikisha mengi kwa lengo jema la kutetea hutu wa mtu mwenye albino.

Akielezea mafaniko kwa sasa nchi yetu yapo yakutosha kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi akuna mauhaji wamependekeza kliniki ziwepo za kutosha.

Mwisho

No comments:

Post a comment