Saturday, 14 March 2020

Makamu wa Rais Samia Aendesha Harambee ya ujenzi wa jengo la CcmNa GUSTAPHU HAULE,PWANI

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu,ameendesha harambee ya ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Pwani na kufanikiwa kupata zaidi ya Sh .milioni 580.

Harambee hiyo ilifanyika jana Mjini Kibaha katika ukumbi wa wauguzi kwa kuwajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunge,wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa dini.

Akizungumza katika harambee hiyo Samia,ambaye pia ni mlezi  wa CCM Mkoa wa Pwani alisema  kuwa ujenzi wa ukumbi huo utakuwa ni mfano wa kuigwa na CCM Mikoa mengine.

Samia,alisema mradi huo ulianza mwaka 2007 lakini ulikwama kutokana na kukosa usimamizi mzuri wa viongozi kwani wengine wao walikuwa wakichumia matumbo yao na hivyo kusahau jukumu walilopewa.

Alisema kuwa, viongozi hao walikuwa wakitumia fedha za ujenzi wa mradi huo kujinufaisha wenyewe lakini hata saruji iliyotolewa na wadau ilifikia hatua ya kuganda lakini hatahivyo anaimani kwa usimamizi wa Sasa mradi huo utafanikiwa.

"Nafahamu kusuasua kwa jengo hilo ni kuwepo kwa usimamizi mbovu lakini kwasasa upo uongozi imara wa CCM na Mimi mwenyewe kwahiyo naimani jengo hilo litakamilika,"alisema Samia.

Samia,alisema kuwa CCM Mkoa wa Pwani haina sababu ya kupita kuombaomba kwakuwa wanamaeneo mengi na mazuri na kwasasa kuna wadau wengi ambao wanaweza kukifanya chama kikajitegemea.

Aidha,katika harambee hiyo Makamu wa Rais alifanikisha kupata zaidi ya milioni 580 ambapo kati ya hizo milioni 113 zilipatikana taslimu huku ahadi ni zaidi ya milioni 471huku akitaka pesa hizo zitumike kwa malengo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, alisema kuwa jengo hilo linajengwa kwa kutumia mfumo wa fosi akaunti(Force Account) na kwamba hakuna fedha ya kupotea.

Ndikilo ,aliipongeza kamati ya usimamizi wa ujenzi huo kwa kuwa wabuni wa kuandaa harambee hiyo huku akimsifu a mwenyekiti wa mstaafu wa CCM Mkoa wa Mara Christopher Sanya kwa juhudi zake za kufanikisha harambee hiyo.

Ndikilo, alisema Sanya licha ya kustaafu kwake nafasi ya uenyekiti lakini amekuwa mwanachama mtihifu wa CCM kwa kufanyakazi kubwa za kukisaidia chama katika shughuli mbalimbali ambapo alimuomba aendelee na jitihada zake za kukijenga chama.

Kwa upande wake Sanya ,alisema kuwa anaimani na CCM kwakuwa ndio chama pekee kinacholeta maendeleo kwa Taifa na Wananchi kiujumla hivyo ni lazima kuunga juhudi za chama Serikali huku akiongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini Rais Magufuli ni mfano wa kuigwa.

Alikishukuru CCM Mkoa wa Pwani kwa kumuamini na kumpa majukumu ya kukijenga chama huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi katika shughuli zote za kujenga chama.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, alisema kuwa jengo hilo linakusudiwa likamilike Juni mwaka huu  ambapo mpaka kukamilika linahitaji milioni 580 na kizuri zaidi pesa zote zimepatikana katika harambee hiyo ambapo aliwashukuru wadau wote kwa kujitokeza.

Hatahivyo,katika harambee hiyo Said Bakhresa aliahidi kuchangia milioni 100 huku Subash Patel akiahidi kupaua jengo nzima linalogharimu milioni 250 pamoja Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyeahidi kuchangia Sh.milioni 50.

Mwisho.

No comments:

Post a comment