
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante
Ole Gabriel akimsikiliza Mkurugenzi wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka
wizara ya Mifugo na uvuvi Dkt.Angello Mwillawa kabla ya kuingia kufungua
kikao cha baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo[LITA] lililofanyika jijini Dodoma.

Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante
Ole Gabriel akizungumza na washiriki wa kikao wakati wa ufunguzi wa
kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo
ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.

Sehemu
ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa
ufunguzi wa kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo
vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.

Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante
Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la
saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA)
lililofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti
wa baraza kuu la wafanyakazi wa wakala wa vyuo vya mafunzo ya
Mifugo[LITA]Dkt.Pius Mwambene,akizungumza kwenye kikao cha Baraza la
saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA)
kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi
wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi
Dkt.Angello Mwillawa,akizungumza kwenye kikao cha Baraza la saba la
wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA)
kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante
Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya
kufungua kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo
vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.
........................................................................................................................
Na.Mwaandishi wetu,Dodoma
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante
Ole Gabriel amewataka Watumishi wa baraza kuu la wakala wa vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuwa chachu katika kutatua changamoto za
wafugaji.
Prof.Gabriel
amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha baraza la saba
la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo[LITA] ambapo
amesema watumishi wa sekta ya Mifugo ni moja ya chachu kubwa katika
kutatua changamoto za mfugaji hapa nchini.
“Ninyi
ni fursa muhimu sana katika kushauri program na kuleta mapinduzi
makubwa katika sekta ya mifugo,hivyo baraza ndio chimbuko la fikra kwa
kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hii ya mifugo na kuwa chachu
muhimu zaidi kutatua changamoto za mifugo hapa nchini”amesema Prof.Gabriel.
Aidha,Prof.Gabriel
amesema watumishi katika sekta ya Mifugo walio na ngazi ya
astashahada[cheti] na Stashahada [Diploma]wamekuwa wakifanya bidii
katika kuwahudumia wafugaji ikilinganishwa na watumishi wenye ngazi ya
Shahada[Degree] kwani baadhi ya watumishi wenye elimu ya juu wamekuwa
wakijiona wako hadhi ya juu kumhudumia mfugaji wa kawaida ,hivyo wakati
umefika kwa watumishi bila kujali elimu waliyo nayo kubadilika na kuwa
karibu katika kumhudumia mwananchi wa kawaida.
Katika
hatua nyingine Prof.Gabriel amesema changamoto inaweza kuwa fursa hivyo
amewataka wafugaji na watanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa na desturi
ya kugharamia na kuhudhuria kozi ya muda mfupi namna ya ufugaji bora
ili kuwa na ufugaji wenye tija.
“Nakumbuka
sitosahau nilipofiwa na baba yangu alikuwa mchungaji,tulinunua jeneza
kwa laki nne,wakati mimi nalia nimepoteza mzee yangu lakini muuza jeneza
ananiambia karibu tena majeneza yapo ,wakati nalia kwa uchungu muuza
jeneza anasheherekea biashara imeenda vizuri ,maana yake ni kuwa
changamoto inaweza kutengeneza fursa hivyo wafugaji ukijinyima kidogo
ulichonacho ili upate mafunzo ya kozi fupi za ufugaji unaweza ukafikiri
unapoteza fedha lakini hii utakuwa unajitengenezea mazingira mazuri ya
kufuga mifugo watakaokueletea faida kubwa”amesema .
Pia
Prof.Gabriel amelitaka baraza hilo kuona namna ya kuondoa utegemezi
kutoka serikali kuu na huku akiitaka LITA kuwa na mahusiano mazuri zaidi
na vyombo vya habari katika kujitangaza kwani vina mchango mkubwa
katika kuinua uchumi kuelekea Tanzania ya viwanda.
Awali
Mwenyekiti wa baraza kuu la wafanyakazi wa wakala wa vyuo vya mafunzo
ya Mifugo[LITA]Dkt.Pius Mwambene amesema kuna changamoto mbalimbali hasa
za miundombinu pamoja na upungufu wa wakufunzi takribani 34 wa afya ya
mifugo huku juhudi zikifanyika ikiwa ni pamoja na ukarabati wa
miundombinu na kubuni biashara ,mafunzo ya muda mfupi kwa wafugaji
katika kukabiliana na changamoto hizo.
Naye
Mkurugenzi wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka wizara ya Mifugo na
uvuvi Dkt.Angello Mwillawa amesema tafiti zimekuwa na mchango mkubwa
katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya sekta ya mifugo kwani husaidia
katika kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto
zinazoweza kujitokeza.
Wakala
wa LITA ulianzishwa Tarehe 1/9/2011 kwa sheria ya wakala wa serikali
Na.30 ya mwaka 1997 na marejeo yake ya mwaka 2007 ambapo kuanzishwa kwa
wakala hiyo kulihusisha vyuo vya mifugo na kubadilishwa kuwa Campus kwa
Muundo wa NACTE ambapo hadi sasa LITA ina jumla ya Watumishi 224 na
Campus zote nchini zikiwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 2700 kwa
wakati mmoja na mwaka huu wanafunzi 3634 Wamedahiliwa na kuwa na ziada
ya wanafunzi 934 sawa na ongezeko la asilimia 34.6%.
Post A Comment: