Friday, 20 March 2020

DEREVA WA BASI LA ISAMILO AFARIKI DUNIA AKIENDELEA NA SAFARI KWENYE BASI


Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.

Akizungumza na MsumbaNews blog, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 majira ya saa nne asubuhi.

"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili wameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.

"Wamefika Tinde saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba.


Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili,dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza.

No comments:

Post a comment