Wednesday, 11 March 2020

CCM YAMLIPIA FAINI DKT. MASHINJI, AKWEPA KIFUNGO

BAADA ya jana, Machi 10,2020 Dkt. Vicent Mashinji kukutwa na hatia  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuhukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 30 ama kwenda jela miezi mitano leo Machi 11 Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam  kimemlipia faini hiyo ya sh. Milioni 30 na kupewa kibali cha kwenda kumtoa gerezani.

Mashinji ambaye awali alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema kabla ya hivi karibuni  kuhamia CCM, pamoja na Viongozi nane wa  Chadema wote kwa pamoja walihukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni 350 au kwenda jela miezi mitano.

Katibu wa Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole amefika mahakamani hapo leo mapema kwa ajili ya kulipa faini hiyo.

Akizungumza mahakamani hapo amesema baada ya hukumu hiyo kutolewa  jana viongozi na wanachama wa CCM Mkoa walinza utaratibu wakutafuta fedha hizo ambapo mpaka kufikia asubuhi utaratibu huo ulikuwa umekamilika na kuwalazimu kufika Mahakamani hapo kwaajili ya kupewa utaratibu wa kulipa .

"Tulifika asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu namna ya kumnusuru ndugu yetu na kifungo, utaratibu ni wa kieletroniki baada ya kupewa control namba tumeenda kuweka fedha benki na  kurudi kwa ajili ya kupewa kibali cha kwenda kumtoa gerezani Mashinji", amesema Polepole

"Tumelipa na kupewa risiti ya Mahakama hatua inayofwata ni kwenda kumtoa gerezani kisha kumkamkabidhi kwa wanafamilia, ni mwanachama wetu mpya anaamini utii wa sheria bila shuruti na kufanya kazi kwaajili ya kuleta maendeleo"

Kwa upande wake mke wa Happiness Mashinji ameishukuru CCM  kwa namna ilivyojitoa na kuonyesha ushirikiano kwa mume wake kwani hakutegemea kama mambo yangeenda haraka kwa kuwa mume wake ni mwanchama mpya.

Mbali na Mashinji , wengine waliohukumiwa ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Katibu Mkuu wa  chama hicho, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Salum Mwalimu, Halima Mdee, John Heche, Esther Bulaya, Esther Matiko, Mchungaji Peter Msigwa.

Mpaka sasa chama cha Chadema kinaendelea  kuchangisha wanachama na wapenzi wake ili kukusanya fedha kwa ajili ya kuwatoa viongozi hao gerezani. 
Katibu wa Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole akiwa na wanachama wa CCM akizungumza mara baada ya kufika katika Makahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo alipofika kwaajili ya kulilipa faini ya Mwanachama Dkt. Vicent Mashinji.

No comments:

Post a Comment