Tuesday, 17 March 2020

BUNIFU ZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE ZAVUTIA WENGI


Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu  (MAKISATU) 2020 yameanza  rasmi leo katika viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.

Akizungumza katika maonesho hayo Kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. James Mdoe amesema  Serikali  inatambua mchango wa wabunifu na lengo ni kuhakikisha ubunifu wa Tanzania unatangazwa kimataifa.

Naye  Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema lengo la Chuo hicho ni
Kuwajengea uwezo wabunifu  kuweza kujiajiri ili
Kuendana na kauli mbili ya serikali ya awamu ya Tano ya uchumi wa viwanda.

Prof. Mwakalila ameongeza kuwa Chuo kinawaandaa wahitimu  kuwa  ujasiriamali.

Nao baadhi ya wananchi waliofika katika banda la Chuo hicho walisifia kazi ya ubunifu ambayo imefanywa na wanafunzi hao, huku wakielezea ubunifu wa gari ambalo linazuia wizi wa mafuta na kuwa ubunifu huo utasaidia kupunguza ajali za moto ambazo hutokana na wizi wa mafuta.

Bunifu ambazo Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinaonesha katika viwanja vya Jamhuri ni pamoja na Ghala la uchafu linalojifungua lenyewe, kujifunga lenyewe na kutuma ujumbe kwa muhusika pindi linapojaa( Smart Dustbin), mfumo wa kuzuia wizi wa mafuta kwenye tanki la gari ( Vehicle fuel theft detection System).

 Bunifu nyingine ni ghala  la uchafu la ndani lenye uwezo wa kuhama lenyewe  kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine( mobile smart dustbin), taa za barabarani zinazoongozwa kwa kutumia simu za mkononii, (Traffick light control by using mobile phone),  mfumo wa kuzuia wizi wa madirishani( Window intruder detection System) na Mfumo wa kusoma vocha kwa wenye uoni hafifu( Air Time order).

Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
17.03.2020

No comments:

Post a comment