Wednesday, 19 February 2020

SHIRIKA LA MAWAKI ,CEFA NA CUAMM LAPONGEZWA KWA MRADI WAKE KUTOKOMEZA UDUMAVU IRINGA

Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Salim Robart akifungua warsha kwa niaba ya Ras Iringa 
 .
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho 

Mratibu wa mradi Tanzania Gabriele  Maneo
.....................

SERIKALI ya  mkoa wa Iringa  imepongeza jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na shirika lisilo la kiserikali la CUAMM ,CEFA na  MAWAKI  kwa  jitihada za kusaidia  kutokomeza  utapiamlo  na udumavu  katika  mkoa  kupitia mradi  wake wa Nourishing  the Future.

Pongezi hizo  zimetolewa leo   mjini Iringa na katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Happines Seneda   ambae alisema kuwa mashirika hayo yaliyopo  chini ya  waziri  mkuu  wa Italia kwa kazi nzuri ya  kusaidia   jamii ya  mkoa wa Iringa  kupitia  mradi wa  Nourishing the Future  kupunguza  tatizo la  utapiamlo na udumavu kwa  watoto jambo  ambalo  ni jema kwa  mkoa na Taifa

alisema itihada  hizo za  kuanzisha  mradi  wa   Nourishing  the Future  katika  mkoa wa  Iringa  kwenye halmashauri  za Kilolo na Mufindi zitasaidia  kwa kiasi  kikubwa  kwenda na kasi ya  uongozi wa  mkoa  katika mapambano  dhidi ya vita ya kutokomeza utapiamlo  na kupunguza  udumavu kwa watoto  chini ya miaka  mitano kutoka asilimia 47  iliyopo  sasa na  kushusha  zaidi  kiwango hicho cha udumavu ndani ya  mkoa .

Seneda  alisema mradi  huo  wa  Nourishing the  future utakaotekelezwa  katika wilaya  mbili  za  Mufindi na Kilolo  ndani ya  mkoa wa  Iringa ,kuwa  ushirikiano mzuri  ambao  CUAMM na MAWAKI  wameonesha  ndani ya mkoa kupitia Halmashauri zake  ni ushirikiano  wa  kupongezwa  kwani  mradi huo jumuishi unahusisha kilimo,afya  na lishe umekuja  wakati ambao mkoa upo katika utekelezaji wa mkabata wa kupunguza udumavu .

"  Ni matumaini yangu  kuwa  mradi  utasaidia  kuboresha   siku 1000 za  kwanza za uhai wa mtoto  pia  tunategemea matokeo mazuri  hasa  katika kiashiria cha udumavu ambacho  ni asilimia 47  isiyokubalika kimkoa  ,ninaomba  nikazie  utekelezaji wa malengo  mahususi ya mradi  ambayo ni  kuongeza uwiano wa watu  wanaotumia mlo  wenye  mchanganyiko  ambapo  kwa sasa  hali  halisi  kwa  watoto  ni asilimia 25 tu ndio  wanapata mlo wenye mchanganyiko wa  vyakula mbali mbali "  alisema

 kupunguza kiwango  cha udumavu  kwa  watoto ,kuboresha  hali ya  lishe  na afya  kwa jamii  iliyo katika mazingira  hatarishi kwani kwa kufanya hivyo  kutasaidia  kwa kiasi kikubwa  kuwa na jamii yenye afya  bora   isziyokuwa nautapiamlo wala  udumavu .

Hivyo  aliwaomba  wadau hao wa  CEFA  kufanya utafiti  wa awali  ili  kujua  hali halisi ilivyo  katika maeneo hayo  ya utekelezaji wa maradi  huo  pia  jamii  ihamasishwe   katika  uzalishaji  na utumiaji  wa mazao ya kilimo  na mifugo  yenye  viini  lishe  kwa  wingi  ili  kuboresha hali ya  lishe  na uchumi wa kaya.

" Suala la lishe  ni mtambuka   ninaomba  tushirikiane  vema    kulitekeleza   ,ushirikishwaji  katika mradi  uratibiwe kuanzia  ngazi ya mkoa hadi vijiji na mitaa na takwimu  zikusanywe  vema ,zichambuliwe  na  zitumike  katika kufanya  maamuzi  na tathimini  za  utekelezaji  zifanyike  ili kujua maendeleo ya mradi na endapo  malengo yanafikiwa  niwahakikishie  tu  wadau wetu   kwamba sisi kama serikali tupo  tayari  kufanya kazi na ninyi na tunawakaribisha  sana  endapo  mtapata changamoto yoyote  ya kiutendaji  tuwasiliane  ili  kuitatua   haraka kabla ya kuathiri  utendaji kazi wenu "

Aidha  aliwataka   watendaji wa mamlaka za wilaya  kuratibu  vema  na kusimamia  afua za sekta  mbali mbali  ili  ziweze  kuonesha matokeo chanya kama   ambavyo  serikali ya  awamu ya tano  chini ya Rais Dkt John Magufuli inavyoendelea   kupigania  maendeleo mbali mbali katika Taifa .

Hivyo  aliomba mradi huo wa Nourishing the  Future  kusaidia   katika kupunguza udumavu  na  kuboresha  hali ya  ulishaji /ulaji  wa  vyakula  mchanganyiko kama ilivyooneshwa katika malengo  mahususi  ya mradi huo.
Meneja  wa  wa mradi  wa CEFA  Giovanni Spata  alisema  kuwa  wao kama  wadau wa maendeleo  nchini wamekuwa  bega kwa bega na serikali ya Tanzania  katika  kushiriki  kuchangia miradi mbali mbali  ya  kimaendeleo  katika maeneo  ambayo  mradi  wao  unafanya kazi na wataendelea  kufanya   hivyo kwani ni  moja kati ya malengo ya miradi yao  kusaidiana na serikali kuwaletea wananchi maendeleo .

Alisema  kuwa     tayari  wamekwisha fanya utafiti kwawilaya zote  ambazo mradi  huo utafanya kazi  na  wanajua  wanashughulika na  watoto  wangapi  wenye  udumavu na utapiamlo hivyo  wanapoanza utekelezaji wa mradi huo  wanaamini kabisa  walengwa  watafikiwa na kunufaika  zaidi na mradi huo .

Awali mratibu wa mradi  huo  wa  CEFA  Tanzania Gabriele  Maneo  alisema kuwa  mradi  huo utafanya kazi katika kata  tatu za  Halmashauri ya  Iringa ambazo ni  Mgama ,Maboga  na Kihanga  wakati  wilaya ya Kilolo mradi utafanya kazi katika kata tano za  Dabaga  Idete , boma la Ng'ombe,Mtitu na Ng'ang'ange  huku  wilaya ya  Mufindi mradi utafanya kazi katika kata  tatu za Mpanda ,Kasanga na Igombavanu   kuwa  jumla ya  vijiji vitakavyofikiwa na mradi huo ni  vijji 45 kwa  maeneo yote

Maneo  alisema utekelezaji wa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza  utapiamlo  na udumavu katika vijiji  vyote  vya  mradi huo pamoja na kuwawezesha  wananchi  kuongeza kasi ya  uzalishaji wa mazao mbali mbali ya chakula ,ufugaji ,elimu na afya

No comments:

Post a comment