Monday, 10 February 2020

POLE POLE AWAPA NENO WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DARASA LA ITIKADI JIJINI ARUSHA

 Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Taifa, ambaye pia ni mlezi wa chama hicho Mkoani Arusha Hamfrey Polepole akizungumza na wanavyuo kutoka katika vyuo mbalimbali Mkoani Arusha katika Darasa la itikadi kwa Wanafunzi wa vyuo na Vyuo vikuu lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Naura Spring.
 Wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbali Mkoani Arusha wakisikiliza nasaha za Katibu wa itikadi na uenezi CCM Taifa,Hamphrey Polepole akizungumza katika darasa la itikadi kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu Jijini Arusha.
 
Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Taifa, ambaye pia ni mlezi wa chama hicho Mkoani Arusha Hamphrey Polepole amewataka wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu Mkoani Arusha kujenga mazoea ya kusoma vitabu mbalimbali vitakavyo wawezesha kupata maarifa juu ya masuala ya kimaendeleo.

Ndg.Polepole ameyasema hayo wakati akizungumza katika Darasa la itikadi kwa Wanafunzi wa vyuo na Vyuo vikuu iliyofanyika Jijini Arusha kwa lengo la kuwapa uelewa wa chama cha Mapinduzi na taratibu zake kwa ujumla ambapo amesema kuwa kusoma kutamuongezea mtu maarifa ya kupata ufahamu wa taarifa mbalimbali zinazohusu chama na serikali.

Aidha Polepole amewataka vijana hao kujenga tabia ya kuwekeza mchango wao katika jamii kabla ya kuwa kiongozi ili kuweza kushawishi watu utakaowaongoza na wasisubirie kuwa kiongozi ndio watoe michango yao kwani watakuwa wanaharibu mwonekano na taswira ya kuwa kiongozi kwa watu utakaowaongoza.

"Lazima vijana awe amejiandaa katika utumishi na uongozi  kwa jamii nakuleta maendeleo kabla ya kugombea ili kuweza kuwashawishi watu watakaowaongoza katika jamii inayokuzunguka hii ni moja ya sifa itakayowasaidia kuwa kiongozi kwa wananchi kukuchagua," alisema Polepole.

Vilevile amesema kuwa ni vyema kama kijana akaanza sasa kutatua changamoto katika jamii yako na asisubirie hadi uwe kiongozi ndio afanye hayo kwani atakuwa anajipunguzia sifa ya kuwaongoza wananchi na wakashindwa kumchagua kwa kukosa sifa ya utumishi kabla ya kuhitaji uongozi.

Pamoja na hayo amewasisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kina lenga kuwataka vijana kuwa na maadili na kutumia mitandao ya kijamii katika kujenga Chama na sio kutumia kughushi habari za uongo.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Jerry Muro amesema kuwa vijana hao wakawe chachu ya ushindi kwa ccm katika Mkoa wa Arusha ili kumuenzi Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri alizofanya za kumaendeleo.

Naye Mwenyekiti wa vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Arusha Baraka Solomon Mungure amewataka wanavyuo hao kuhakikisha wanatumia fursa wanayoipata kwa maslahi ya wananchi pia wawapuuze watu wachache wanaoharibu sifa ya chama hicho.

No comments:

Post a comment