Afisa mradi,  Bwana Hasasan Rasuli kutoka Shirika la Medo akielezea lengo la mradi huo.
 Mwalimu Bernard Muna mwalimu wa kitengo maalum kutoka Shule ya Msingi Mchanganyiko Mtinko akitafsiri wakati wanafunzi walipokuwa wanataja haki zao na kuelezea umuhimu wa kodi kwa jamii.
 Wanafunzi wakitaja haki za kumi za watoto.
 Wanafunzi wakiendelea na kutaja haki za watoto na umuhimu wa kulipa kodi.
 Maswali yakijibiwa.
Wanafunzi wakiimba wimbo unaohamasisha jamii kutambua umuhimu wa kulipa kodi.
Na Mwandishi wetu, Singida
WANAFUNZI katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wamejengewa uwezo wa kutambua haki zao za msingi ikiwemo elimu na umuhimu wa jamii kulipa kodi itakayo saidia serikali kutatua changamoto mbalimbali lengo ni kuwa na jamii yenye uelewa huo hapo baadaye.
Shule ya Msingi mchanganyiko Mtinko ni moja ya shule zilizofikiwa na mradi wa kuwajengea uwezo wanafunzi kujua haki zao na umuhimu wa kulipa kodi mradi unaotekelezwa na Shirika lisilokuwa la serikali la Mtinko Education Development Organisation (MEDO) katika shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Singida,ambapo wanafunzi hao walisema kwa sasa wamefahamu haki zao ikiwa ni pamoja na kutobaguliwa na haki ya kupata elimu katika mazingira bora na umuhimu wa jamii kulipa kodi
Walisema awali walikuwa hawaoni umuhimu wa kodi na haki za msingi za watoto lakini baada ya kufundishwa na Shirika hilo wameona kumbe kuna umuhimu mkubwa wa jamii kulipa kodi na kuwapa watoto haki zote zinazohitajika kwao na kwamba hata watoto wenye ulemavu nao wana haki hizo,huku wakiiomba serikali kuendelea kuboresha Miundombinu ya shule hasa kwa upande wa watoto wenye ulemavu ili waweze kupelekwa shule kwani wengi wao bado wako majumbani.
Afisa Mradi wa Shirika hilo Hassan Rasuli alisema wao kama Shirika wameona kuwekeza kwenye elimu ya kujua haki za msingi na kodi kwa wanafunzi ili kuwa na jamii yenye uelewa na hiyo ndio mbinu tuliyoina inafaa kwa kuwekeza jambo kwa watoto baadaye wakikua watakuwa na uelewa,serikali haitahangaika kutoa elimu hiyo kwani tayari jamii itakuwa nayo.
Rasuli alisema kwa sasa wanatekeleza mradi huo kwenye shule 17 za Msingi na shule 2 za Sekondari katika Halmashauri hiyo ambapo mbali na kuwajengea uwezo wanafunzi pia wamekuwa wakiwashirikisha wanafunzi kwenye vikao mbalimbali vya kijamii kama vile vikao vya kamati za shule na vikao vingine vya kijamii vinapofanyika kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za wanafunzi.
"Naiomba jamii mtambue wajibu wenu kwa watoto hawa kwani bila sisi wazazi kushiriki kikamilifu watoto wetu wataendelea kupata shida,hawatapata elimu kwenye mazingira yalio bora." alisema Rasuli
Aidha akitoa taarifa ya Shule hiyo ya Mtinko Mwalimu Rahel Msanga alisema Shule hiyo inafundisha wanafunzi wenye uziwi na wasio na ulemavu lakini inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa,walimu wa vitengo maalumu kwani kwa sasa wapo walimu wawili pekee kati ya walimu 20 wanaofundisha Shuleni hapo,hivyo naiomba Serikali itusaidie kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na walimu ili kuondoa changamoto hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: