Monday, 24 February 2020

KUTOPITIWA KWA MISWADA YA JINSIA NA MADINI BADO NI CHANGAMOTO YA MTANGAMANO


Na Ahmed Mahmoud Arusha
Spika wa county ya Kajiado nchini Kenya Johnson Osoi Amewataka marais wa Jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia namna jinsi ya kuwezesha kupitiwa sheria  kusainiwa kwa miswada ya sheria kwa mawakili kufanyakazi kwenye mataifa yote bila vikwazo.

Pia Muswada wa jinsia na muswada wa sheria ya madini kwenye nchi za jumuiya ambao umekuwa ukisuasua bila kupatiwa ufumbuzi na
Bunge la Afrika mashariki.

Uwepo wa sera sheria ya madini ya jumuiya hiyo ambayo itasaidia mataifa hayo kuweza kunufaika na kuwesha kuilinda rasilimali hiyo kwa pamoja katika ukanda wetu tukiwa na sheria moja kama mataifa ya jumuiya.

 Imeonekana kwa Sasa kila nchi imekuwa  hawaitaki kuisikia kila mmoja anahitaji kusimama na sheria yake badala ya kuwa na sheria moja ya Eac kwenye sekta ya madini.

Hadi Sasa ni Muswada Muswada wa makubaliano ya kufanyakazi za kisheria ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki ambayo haiukusainia wa wanasheria wa nchi jambo linalowanyima fursa ya kufanyakazi zao kwenye nchi hizo tofauti na Sasa anafanyakazi ndani ya nchi yake pekee.

Akizungumza kwenye semina ya siku nne iliyolenga kujadili sera sheria kwenye mtangamano wa jumuiya ya Afrika mashariki iliyoandaliwa na EALS chama cha wanasheria wa nchi hizo Spika huyo alisema kuwa msingi mzuri ni marais kupitisha sheria ambayo hadi Leo haijafanyiwa kazi imeishia bungeni na washeria wakuu wameshindwa kuisaini hadi sasa .

Alisema kuwa nchi hizo na sheria hizo zitasaidia kuongeza tija na mtangamano 
katika kuhakikisha wananchi wanajenga faida na uelewa wa kisheria kwa Mawakili wetu kuweza kwenda kufanyakazi maeneo yote ya nchi hizo.

"Unajua sheria ya Mawakili kuweza kwenda na mtangamano wa nchi zetu inahitaji kuisaidia jamii na Marais wetu mna jukumu ya kuhakikisha sheria yetu iliyokwama inafanyiwa kazi kusaidia uandaaji wa sera na sheria hiyo inafanyika kama ilivyoombwa awali"

Kwa upande wake Afisa Mipango Sera na uhusiano wa EALS David Sigano alisema kuwa sheria hiyo imekwama hadi leo kwenye bunge la Afrika Mashariki na hawajui ni lini bunge litaipitia sheria hiyo ili kuwezesha Mawakili kufaidi mtangamano wa Afrika mashariki.

Alieeleza kuwa chama hicho kimekuwa  kikisimamia kuona nchi hizo zikisimamia sheria na utawala Bora kwa kutoa ushauri wa kisheria ikiwemo mipango ya kuendeleza dhana nzima ya kisheria inapewa kipaumbele na mataifa yetu l.

"Naona ni muhimu Sana nikakumbushia muswada uliopo bunge la Afrika mashariki EALA kwa muda Sasa bila kuwa sheria inayowatambua Mawakili kuweza kwenda kufanyakazi kwenye nchi zetu jambo hili tunaomba lifanyiwe kazi haraka kama zilivyo taasisi nyingine"

Kwa mujibu wa sheria hiyo ambayo imekwama hadi leo kwenye bunge la Afrika mashariki ambayo chama hicho kwenye semina hiyo kinatoa mafunzo ya sera na sheria mbali mbali ili kuendelea kuboresha matangamano huo kwa viongozi kutoka kada za Serikali na binafsi.

No comments:

Post a comment