Vijana Mkoani Kagera wametakiwa kuondokana na  kutegemea ajira toka serikalini badala yake wajijengee mazingira ya kuwezeshwa kwa kukaa katika makundi ili wanufaike na fursa mbali mbali zitolewazo na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, Ajira, Sera na watu wenye ulemavu Mhe, Anthony Mavunde katika Kongamano la Umoja wa vijana CCM mkoa wa Kagera chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Ndg Happiness Runyogote katika ukumbi wa Linas uliopo manispaa ya Bukoba Mkoani humo.

Akizungumza na vijana hao walikiwemo wenye ulemavu Mhe, Anthony Mavunde amesema anatambua moja ya changamoto ya ukosefu wa kipato na ajira na kuwa si kila mmoja anaweza kuajiriwa katika sekta rasmi bali vijana wanapaswa kuondokana na utegemezi wa ajira badala yake wajitengenezee makundi yatakayowawezesha kupata fulsa mbali mbali kwa uraisi.

Amesema “Vijana wanaamini kuwa
ajira ni kukaa maofisini wakati wapo vijana waliofanikiwa kupitia kilimo, uvuvi hata kujiajiri katika biashara ya kuuza matunda na kupata mafanikio.”

 Waziri Mhe Mavunde amesema serikali inathamini vijana na imeweka mipango kabambe ya kuwasaidia vijana ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa makundi katika jamii, wenye ujuzi, wasio wajuzi, walioishia darasa la saba, wenye ulemavu, wenye vipaji na katika hatua ya Elimu, kujikusanya katika mfumo wa vikundi ili waweze kunufaika na fulsa mbali mbali.

"Ajira sio ofisini vijana nawahimizeni tengeneza mazingira ya kuwezeshwa fulsa haina mataili kuwa ikufuate ulipo badala ya kuilaumu serikali kaeni katika makundi fulsa zitawakuta " alisema Naibu waziri huyo.

Amesema vijana lazima wafanye biashara halali na yenye kuwaingizia kipato ili wakipewa nguvu wawe na kianzio.

Aidha amesema wananchi wenye uwezo wa kufanya kazi hapa nchini kuanzia miaka kumi na tano ni milioni 24.3 huku akieleza kuwa ifikapo mwaka 2021 vijana milioni 4.4 watahitajika.

Kwa upande wa Mbunge wa Vijana Mkoani Kagera Mhe @halima_bulembo amesema atahakikisha anatoa ushirikiano kwa vijana huku akiwahimiza kutobagu kazi.

Pia Ndugu @Joanfaith_john ambaye ni mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa amewasihi vijana kufanya kazi na kubadilika
Share To:

msumbanews

Post A Comment: