Sunday, 2 February 2020

GCLA KANDA YA KASKAZINI YATOA VIBALI 2,172 VYA MATUMIZI YA KEMIKALI


NA ANDREW CHALE, ARUSHA

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Kanda ya Kaskazini imeweza kutoa vibali mbalimbali vya kutumia kemikali kwa waombaji 2,172.

Hayo yalielezwa na Meneja wa GCLA kanda ya Kaskazini Christopher Anyango kufuatia kampeni ya Tumeboresha sekta2.1 ya afya inayolenga kuonyesha mipango na mafanikio ya taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Kampeni hiyo inafuatia ziara ya Maofisa Mawasiliano kutoka wizara ya afya pamoja na taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.

Anyango alisema GCLA kwa mwaka 2016,2017 wametoa vibali 2,000 lakini kwa mwaka 2019,2020 walitoa vibali 2,172.

"Kwa mwaka 2016,2017 uthibiti wa kemikali haukuwa wa kiwango kikubwa kwasababu tulikuwa na mtumishi mmoja pekee aliyekuwa katika mpaka wa Namanga ,uingizwaji wa kemikali ulivyoongezeka, serikali ilitutengea bajeti iliyotuwezesha kuajiri watumishi, ambao wapo katika mipaka kanda ya kaskazini" alisema.

Anyango alisema ongezeko la upimaji wa sampuli kumechangiwa vile vile na uimarishwaji wa ukaguzi.

"Pia kwa mwaka 2016,2017 viwanda vilivyosajiliwa kushugulika na kemikali ni 100 lakini sasa 2019,2020 tumesajili viwanda 250, kwa hiyo katika kipindi cha Rais Dk.Magufuli tumesajili viwanda 150" alisema.

Akizungumzia maboresho ya GCLA alisema wameboresha mfumo wa utoaji wa vibali kwanjia ya mtandao jambo linalorahisha utoaji wa vibali pamoja na ukaguzi.

"Hakuna  watu wanaokuja ofisini kwetu kuomba vibali bali wanaingia kwenye mtandao na kuomba vibali, ndani ya muda mfupi tunaangalia ombi lake na kupata majibu kwa muda mchache" alisema.

"Pia tuna mpango wa kuanza kupima sampuli zote zinafikishwa hapa kwa wingi " alisema.

Kwa upande Mtaalamu wa Maabara Saile Maregesi alisema  maabara ya GCLA kanda ya kaskazini imekuwa msaada mkubwa katika kusaidia upimaji wa sampuli za seli kwa watu waliofanyiwa ukatili.

"Mfano mtu aliyebakwa kuna seli zinabaki katika mavazi kwahiyo tunachofanya tunachukua seli za huyo aliyebakwa na mmbakaji ndio maana wanaobakwa tunashaurigi wasioge" alisema
Mwisho.

No comments:

Post a comment