NA HERI  SHAABAN

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu amezindua kampeni ya Kipepeo mkoani Morogoro.

Akizindua kampeni hiyo Waziri Ummy alisema kampeni hiyo ya kipepeo inatekelezwa kwa ushirikiano wa wizara ya afya Jinsia na Watoto kupitia  Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI  (NACP)  na Taasisi ya Benjamin Mkapa.

Ummy alisema dhumuni la kampeni hiyo kuwasaidia wanafunzi hasa wa kike kujitambua, kujiamini, na kuongeza bidii ya kujenga ndoto zao sambamba na kuwapatia mbinu namna ya kupambana na changamoto za kimaisha, kimasomo na vishawishi zinazoweza kuwapotezea ndoto zao.

"Napongeza Wizara yangu  kwa kushirikiana na taasisi na wadau  wa afya lengo la kuifanya kampeni  hii kuwa kubwa ili kuwafikia wengi zaidi wa lika la Balehe  wanaosoma shule za sekondari kwa ajili ya kuwafikishia  Elimu kuhusu  maambukizi ya Virusi vya UKIMWI  (VVu) "alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy alisema athari za mimba za utotoni ,matumizi sahihi ya ARV kwa wale walioathirika tayari sambamba na kueneza elimu dhidi ya unyanyapaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa alisema kampeni ya kipepeo itafanyika kwenye jumla ya mikoa kumi (10) ambapo vigezo vya kuchagua Mikoa husika ni viwili; kwanza ni kwa kuzingatia mikoa yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU kwa kundi linalolengwa.


 Aidha aliema , mikoa yenye kiwango cha juu cha mimba za utotoni. Mikoa hiyo ni pamoja na Mbeya, Iringa, Njombe, Mwanza, Dodoma, Tanga, Arusha, Mtwara, Morogoro na Singida.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Laota Ole Sanare alisema Mkoa wake unaunga mkono Kampeni hiyo kwakuwa kupitia kampeni kama hizo Mkoa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), athari za mimba za utotoni, matumizi sahihi ya ARV kwa wale walioathirika tayari sambamba na kueneza elimu dhidi ya unyanyapaa.
  MWISHO
Share To:

msumbanews

Post A Comment: