Waziri wa mariasili na Utalii Dkt, Khamis Kingwangalla akipewa heshima ya kimasai 
Waziri wa mariasili na Utalii Dkt, Khamis Kingwangalla akivishwa vazi la heshima
Wananchi wakimsikiliza waziri Dkt Kigwangala 

NA HERI  SHAABAN

WAZIRI wa Mariasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangala amechangisha shilingi milioni 117 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Ketumbeine Wilayani Longido.

Akiongoza harambee hiyo mwishoni mwa wiki Waziri Kigwangala alisema afya ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu ndio maana tumevuka lengo lililokusudiwa lengo lilikuwa shilingi milioni 100.

Waziri Kigwangala alisema harambee hiyo imehusisha wananchi wa eneo hilo wa kabila la Masai ,ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Steven Kiruswa ,viongozi wa halmashauri ya Longido ,mashirika, wadau wa maendeleo na taasisi za hifadhi  zilizo chini ya Wizara ya Mariasili na utalii .

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala ambaye alikua mgeni rasmi amewapongeza wananchi wa Kata hiyo kwa  kujitolea na kuwataka waendelee kushiriki na  kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo inayoanzishwa na kutekelezwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt.John  Magufuli.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza wananchi hao kuwa Serikali ya awamu ya tano imekua ikitekeleza na kukamilisha kwa vitendo miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, miradi ya maji, umeme na huduma za afya, elimu.

Dkt. Kigwangalla alisema  kupatikana kwa fedha hizo kutawawezesha wananchi wa kata hiyo kukamilisha jengo la kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje, kuwezesha upatika aji wa huduma za upasuaji, huduma ya mama na mtoto hivyo kuondoa adha ya muda mrefu ya wananchi  kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 90 kufuata huduma za afya.

" Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli ni Serikali inayoahidi na kutekeleza, haya yote yanayofanyika ni kwa sababu Rais wetu anachapa kazi,  nawaomba muendelee kumuunga mkono na kumuombea dua Rais wetu ili aendelee kutetea maslahi ya wananchi"alisema Dkt.Kigwangalla.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Steven Kiruswa akizungumza mara baada ya kukamilika kwa harambee hiyo amemshukuru Waziri Kigwangalla kwa kuwaunga mkono wananchi wa Kata ya Ketumbeine ambao kwa asili ni Wafugaji na wahifadhi wa wanyamapori kwa kuwa eneo wanaloishi lina wanyamapori wa aina mbalimbali.

Alisema kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha kazi ya ujenzi ikamilike na kuwawezesha wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu hasa Mama wajawazito na watoto kuanza kupata huduma za afya  karibu.

Kwa upande wao wanannchi wa Kata hiyo wakizungumza kwa nyakati wameeleza  kukamilika kwa kituo hicho ni ukombozi kwao na kwa wananchi wa maeneo ya jirani waliokua wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Wameeleza kuwa wao kama wafugaji wanaoishi katika eneo hilo ambalo lina wanyamapori wa aina mbalimbali wataendelea kuwa mstari wa mbele kulinda na kuhifadhi rasirimali na mariasili zilizopo katika eneo lao.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: