Mkuu wa Mkoa Iringa Ally Hapi ameanza harakati za kutafuta wawekezaji wa sekta ya Utalii kuja kuwekeza ndani ya mkoa wa Iringa mwandishi Humphrey Kisika anaripoti toka Tarangire .

Kuwa Hapi ametoa Rai hiyo leo wakati wa   kikao kati yake na  wawekezaji wakubwa wa Utalii kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire

 Hapi alisema kuwa ni furaha kubwa sana kufanya kikao hicho chenye tija na kutangaza fursa za Uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Iringa.

Alisema mkoa wa Iringa  Kuna maeneo ambayo tayari yamekwisha tengwa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Utalii, kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Pia Kuna ofisi maalumu inayo shughulikia maswala ya uwekezaji na kumsaidia mwekezaji kukamilisha malengo yake kwa haraka zaidi pasipo usumbufu wowote ule, ofisi hii inapatikana kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Alisema ofisi yake inafanya inaendelea kufanya mazungumzo na shirika la ndege la kampuni ya Auric Air, ili waanzishe ruti Iringa, dodoma, Arusha na Zanzibar. Hii itasaidia sasa kurahisisha usafiri kwa mtalii na wadau wengine.

Hapi alisema kama .koa  umejipanga kuwekeza Utalii katika mashamba ya miti yaliyopo Sao hill kwa kujenga hotel ndani ya misitu ili kuonesha uzuri wake, pamoja na mashamba ya chai, ikiwa na kutumia uwanda wa maji ulipo maeneo ya Sao hill kwa Uvuvi.

Mhifadhi mkuu msaidizi wa Tarangire ndugu Gala, akichangia katika kikao hicho amesema kuwa kupitia ziara hii ya Mhe Hapi na wataalamu wake amejifunza vitu vingi mno, lakini kubwa zaidi amefurahishwa sana na uhamuzi wa Mhe Ally Hapi, kutoka ofisini kwake na kuanza kutafuta na kutangaza fursa za uwekezaji ndani ya Mkoa wake hii inatia hamasa sana hasa kwa Wawekezaji hao, kweli Mkoa wa Iringa umeamua kwa dhati kutangaza vivutio vilivyomo ndani ya Mkoa huo. Amesema siyo dhambi na viongozi wengine wakaiga ufanyaji wa kazi Kama wa Mhe Hapi, na siyo kukaa ofisini tu.

Wadau wa utalii Iringa walisema  Iringa ina fursa nyingi sana za Utalii, ila itapendeza sana Kama kutakuwa na Utalii wa kutembea kwa miguu hasa katika kupanda mlima Kitonga, lakini serikali inayo jukumu la kuongea na mwekezaji wa hotel ya kitonga na ile ya Mamba iliyopo Ruaha Mbuyuni, hizi zitasaidia Sana kufungua Utalii ili anapokuja mtalii apate fursa ya kukaa muda mrefu Iringa, tofauti na sasa vivutio vipo mbali na hifadhi ya Ruaha.

Afisa utalii na maliasili Bi, Hawa Mwechaga, akiwasilisha Taarifa ya uwekezaji katika maeneo yaliyotengwa na Utalii kwa ujumla, amesema Iringa ina Utalii mkubwa sana na watofauti tofauti ikiwa wa kimila na desturi

Hapi amewaambia Wawekezaji hao kuwa Ofisi yake na wataalamu wamejipanga vizuri sana hivyo akuna ubabaishaji kabisa waje hata kesho.

Hapi na wataalamu wake wamefanya ziara siku mbili katika Mkoa wa Manyala, na ametembelea Wawekezaji wengi. Na leo anaelekea Arusha.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: