Mbunge wa Mwibara na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili makao makuu ya ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa.

Lugola amefika katika ofisi hizo leo Ijumaa Januari 30, 2020 saa 1.24 asubuhi akiwa katika gari ndogo aina ya Klugger rangi nyeusi na hakuingia nayo ndani ya geti. 

Mmoja wa maofisa wa Takukuru amesema baada ya Lugola kuhojiwa, saa 3.30 atahojiwa aliyekuwa Kamishina wa Zimamoto, Thobias Andengenye, saa 8.00 atahojiwa aliyekuwa Katibu Mkuu, Jakob Kingu ambaye sasa ni balozi na saa 12 jioni atahojiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.

Kuhojiwa kwa watumishi hao ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu mkataba tata walioingia katika manunuzi ya vifaa vya zimamoto.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: