Mkuu wa wilaya ya Mbarali Rubein Mfune (kushoto) akikabidhi  mifuko ya unga wa msaada  kwa viongozi wa  Igawa

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Rubein Mfune akishiriki kubeba mifuko ya unga alitoa msaada msaada  kwa wananchi wa Igawa

Na Esther Macha, Mbarali

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya  Reuben Mfune ametoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya shilingi million 5.1 kwa wakazi 208 wa kata ya Igava kijiji cha Igava ambao wameathirika  na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani hapa.

Mfune ametoa msaada huo wa vyakula Leo wakati alipokwenda kuwajulia hali pamoja na kutekeleza ahadi aliyoitoa  Desemba 31.mwaka jana.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ,Kivuma
msangi ametoa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni tano na laki moja ambavyo bado havijakidhi majitaji.

Msangi alisema kuwa ingawa msaada huo ni mdogo ila utasaidia kusukuma siku Huku juhudi zingine zinaendelea za mipango .


Naye Mratibu wa Maafa Wilaya ya Mbarali,  Zabron Abel amesema kwamba mvua zilianza kunyesha desemba 29 katika Kata ya Igava.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Igava ambao makazi yao yameathirika wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwasaidia chakula kwa wakati kama alivyoahini ambapo chakula hicho kitawasaidi kwa siku kadhaa huku wakiwa wanajipanga kujitafutia chakula na makazi mengine.

Mkuu wa wilaya ya mbarali amekabidhi unga wa sembe kilo 1050, mchele kilo 1050, maharagwe kilo 480, chumvi pakti  208 na mafuta ya kupikia lita 208 ambapo vyakula hivyo vitagawiwa kwa wananchi 208 wa kijiji cha Igava ambao nyumba zao zimeharibika kwa kiasi kikubwa na kwa kila mmoja wao atapata kilo 5 za unga wa sembe, kilo 5 za mchele, kilo 2 za maharagwe, pakti moja ya chumvi pamoja na mafuta lita moja.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: