Saturday, 21 December 2019

WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA KWA KULA MHOGO NA KISAMVU


WATU  watatu amefariki dunia mkoani Manyara katika matukio tofauti likiwemo la
watoto wawili wa Familia moja katika kijiji cha Gidas,Wilaya ya Babati mkoani kufariki baada ya kula Mhogo na kisamvu vilivyodhaniwa kuwa na sumu .Mwandishi wetu John Walter anaripoti kutokaManyara


Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Manyara (SACP) Paul Kasabago amewataja waliofariki kuwa Bashiru Hamad (6) na mdogo wake Mwanahamisi Hamad (4).

Waliodhurika na mihogo hiyo ni mama wa watoto Christina Joseph (28),Selina Safari (41) pamoja na Paulina Bura (19) na wote wanaendelea vizuri.

Katika tukio lingine Desemba 18.2019,huko katika kijiji cha Taigo kata ya Ngigirish Tarafa ya Matui wilaya ya Kiteto mkoani hapa, msichana aitwaye Sara Msimba (10) mwanafunzi wa shule ya Msingi Taigo,alifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye Kisima wakati anachota Maji.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo aliondoka nyumbani majira ya saa 10:30 Jioni kuelekea kisimani akiwa na Galoni lakini hakufanikiwa kurudi tena hadi wazazi wake walipopatwa na wasiwasi wa kumfuatulia na kukuta galoni pembeni mwa Kisima ndipo wakaanza jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na majirani waliotoa maji yote kisimani na kuukuta mwili huo.

No comments:

Post a comment