Afisa maendeleo wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Naftari Sailoy


                         Afisa maendeleo wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Naftari Sailoy akizungumza kwenye mkutano wa 27 wa Saccos ya watumishi wa manispaa hiyo


Wanachama  wa chama cha kuweka na kukopa [Saccos ] ya watumishi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wedaiwa  wa mikopo ya chama hicho wametakiwa kurejesha mikopo hiyo ili na wanachama wengine waweze kukopa .

   Afisa maendeleo wa Manispaa ya Songea Naftari Sailoy ametoa rai hiyo jana  wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa 27 wa chama hicho ambacho kinazaidi ya wanachama 285.

  Sailoy ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo amesema kuwa watu wamekuwa wakiwakwamisha wanachama wengine  kukopa kutokana na kutokurejesha madeni yao ya mikopo.

  Alisema kuwa kuanzia sasa waanze kufuatiliwa ili waweze kurejesha madeni hayo na ikiwezekana ufanyike utaratibu wa kisheria ambao utakaowafanya walipe na kukifanya chama kiendelee kuwa na uhai wa kuwahudumia wanachama wake.

   Kwa upande wake Afisa ushirika wa Manispaa hiyo Given Mariki awali amesema kuwa baadhi ya wadaiwa sugu hao wamekuwa wakitoa lugha za kejeri pindi wanapoambiwa walipe madeni ambayo wamekuwa wakidaiwa na Saccos hiyo.

  Mariki ambaye ni mlezi wa Saccos hiyo amesema baadhi yao wamehamishwa kikazi wapo nje ya Manispaa hiyo, huku wakiwa wamehama  na madeni jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma jitihada za maendeleo ya chama.

   Naye mwenyekiti wa chama hicho Idd Waziri amesema kuwa licha yakuwepo kwa changamoto hiyo lakini bado chama kinajitahidi kuendelea kutumia fedha zake bila mikopo ambapo hadi sasa ni zaidi ya milioni Mia tano [500]zipo.

  Waziri amewaomba wanachama hao kueendelea kuwa waaminifu wa kurejesha fedha walizokopa maana uhai wa Saccos yeyote ni kufanya marejesho kwa wakati na siyovinginevyo.

“Jamani marejesho ndiyo moyo wa Saccos yeyote ile hivyo ni vema kila mwanachama ajionje kuwa anawajibu wakurejesha madeni ili na wengine wapate kunufaika “amesema mwenyekiti Idd Waziri.

  Katika mkutano wa chama hicho wanachama wapya 20 wameweza kujiunga na Saccos huku baadhi ya wanachama wanachama ambao wamefanya vizuri katika mikopo yao wameweza kupata tuzo ya sh.100,000.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: