Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza na wananchi wa kata ya Msindo Wilaya ya Namtumbo wakati akizindua mchakato wa ujenzi wa kituo cha Afya katika kata hiyo ambacho zaidi ya Sh.400 zimetengwa 

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezitaka kamati zitakazoundwa wakati wa ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Msindo Wilaya ya Namtumbo ziweze kulinda vifaa vya ujenzi visiibiwe ili kufanikisha ujenzi huo kwa wakati.Mwandishi Amon Mtega anaripoti toka Namtumbo Ruvuma

 Wito huo aliutoa  wakati akizindua mchakato wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya kitakachojengwa katika kijiji cha Mtakanini kata ya Msindo ambapo fedha zaidi ya Sh.Milioni 400 zimetengwa kwaajili ya ujenzi huo.

  Mndeme amesema kuwa ili kufanikisha ujenzi huo na kuufanya uende haraka ni lazima kamati ziweze kuvilinda vifaa ambavyo vimenunuliwa kwaajili ya shughuli hiyo na kuachana na tabia za baadhi yao kufanya udokozi [Wizi] maana kufanya hivyo kutaifanya kituo hicho kushindwa kukamilika kwa wakati.

 Amesema kuwa kituo hicho ambacho majengo yake yatajengwa ya kisasa kitakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo ambayo ina vijiji vinne[4] hivyo  watu ambao watakaofanya ubadhilifu hawatavumiliwa.

 “Kituo  hiki kitakuwa ni ukombozi mkubwa na kitaanza na majengo sita [6] ambayo ndani yake kutakuwepo jengo la mama na mtoto ,upasuaji ,Chumba cha kuhifadhia watoto njiti,sehemu ya kuchomea taka  na mawodi mengine ya kulazia wagonjwa”alisema mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.

  Kufuatia hali hiyo mkuu huyo amesema kuwa ofisi yake haitavumilia wanakamati ambao watafanya ubadhilifu na kuwa watachukuliwa hatua zinazostahiki ili iwe funzo kwa wengine.

  “Haiwezekani Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli atupatie fedha kwaajili ya kujenga kituo cha Afya ili wananchi waweze kupata huduma halafu watu wengine wanataka kuweka sehemu ya kujinufaisha nasema sitakubali hilo na watapigwa kata funua”alisema Mndeme .

 Kwa upande wake mmoja wa wanakijiji hicho Remna Nchimbi ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia fedha hizo za ujenzi wa kituo cha Afya ambapo awali walikuwa wakipata shida hasa wakinamama ambao wengi wanadaiwa walipoteza maisha kwa kujifungulia njiani wakati wakifuata huduma ya matibabu katika Hospital ya rufaa  ya mkoa Ruvuma.

                                     
.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: