Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi (kulia)akitoa maelekezo kwa mafundi wanaojenga Hospitali ya wilaya ya Iringa  mwenye suti nyeusi kushoto katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happines Seneda 

...............
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Hapi, ametoa siku tatu (3) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa iwe imekamilisha ujenzi wa Hospitali wilaya inayojengwa eneo la Igodikafu.

Mhe Hapi, ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo kimsingi ilipaswa kumalizika  toka mwezi uliopita kwa maagizo ya Waziri wa TAMISEMI Mhe Suleman Jaffo, aliyoyatoa wakati wa ziara yake alivyotembelea Hospitalini hapo.

Pamoja na kuagiza ujenzi huo kukamilika hadi Desemba 3 mwaka huu pia Mkuu wa Mkoa ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata Mafundi wa kuu watatu (3) ambao wamekwishalipwa fedha zao na hawaonekani eneo la kazi kukamilisha kazi hiyo ya ujenzi .

"Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa nakuagiza hawa mafundi watatu ambao hawapo katika eneo la kazi na fedha wamelipwa watafutwe na wapelekwe mahabusu, Kisha wapelekwe kuendelea na kazi wakitokea mahabusu na watafanya kazi usiku na mchana kwa usimamizi wa Jeshi la Polisi kuanzia leo " alisema Mhe Hapi.

Kwa kuwa serikali ya Mhe, Rais Dkt John Magufuli imetoa fedha kiasi Cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ili Wananchi wapate huduma za afya hivyo Uongozi wa Mkoa hautakubali kuona mtu anacheza na fedha hizo za serikali "

Wakati huo huo Mhe Hapi, ameagiza Jeshi la Polisi kupeleka askari wa FFU na wale wa JKT ili kusimamia ujenzi huo huku akimtaka Mganga Mkuu wa Wilaya na wote wanaohusika na usimamizi wa Hospitali hiyo kushinda eneo la ujenzi huo .

Katika hatua nyingine Mhe Hapi, amepongeza ujenzi wa mradi wa Maji unaoendelea Kijiji Cha Magombwe na Igodikafu kuwa ni miradi inayoenda vizuri .
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: