Thursday, 26 December 2019

Mume mwimba kwaya aua mkewe kwa Shoka


Mwanamke mkazi wa kijiji Kilanga wilaya ya Arumeru Marry Richard Mushi mkazi wa ameuawa kwa kupigwa na shoka na mume wake wakati akijiandaa kuanza sikukuu ya Krismas. 

Tukio hilo wakati wakiwa katika  maandalizi ya sikukuu ya Krismasi disemba 25 mwaka huu majira ya mchana kuwa mwanaume huyu Moses Latiaeli Pallangyo maarufu kwa jina Moses Lebaba ambae ni mwimbaji nyimbo za injili. 

Imeelezwa kuwa tukio hilo limetoka ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mtuhumiwa kama mke na mume ambapo baba wa mtuhumiwa mzee Latiaeli samson Pallangyo alisema hapakuwa na ugomvi wowote na walitegemea mauwaji hayo . 

"Wawili hao walikuwa wakijiandaa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kuwa Marry alipika chai na kisha kuendelea na shughuli za kawaida kabla ya kupigwa na shoka akiwa chumbani Kweke akijiandaa kusherekea sikukuu " 

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru Jerry Muro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo . 

Muro alisema baada ya taarifa hiyo kutoka kwa wasaidizi wake katika ulinzi alifika katika eneo la tukio muda mchache baada ya tukio. 

Pamoja na kutoa pole kwa familia ya marehemu na wananchi wa kijiji cha kilinga kwa tukio hilo la kikatili lilitokea alisema tayari vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimeanza msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake. 

Muro aliwataka wananchi wenye kujua taarifa za alipokimbilia mtuhumiwa wasaidiane na vyombo vya usalama kumsaka ili sheria iweze kuchukua mkondo wake .

 Aidha alisema hata kibali kuona vitendo vya kikatili kama hivyo vikijitokeza katika wilaya yake

No comments:

Post a comment