Friday, 6 December 2019

MSAFARA WA DC WA KILOLO WAJERUHIWA KWA NYUKI ,MWENYEWE ATIMUA MBIO


Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdallah akijiandaa kutimua mbio wakati akikagua mradi wa ufugaji nyuki kijiji cha Lulindi kata ya Ukwega baada ya nyuki kuwajeruhi watu watatu wakiwemo waandishi wawili wakati akikagua mradi huo 
Waandishi wa habari na wananchi wakimbia  baada ya kushambuliwa na nyuki 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo na msafara wake wakianza ukaguzi wa mradi wa ufugaji nyuki kabla ya nyuki kuwafukuza

...................................................................
MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa Asia Abdallah na msafara wake walazimika kutimua mbio na kuahirisha zoezi la ukaguzi wa mradi wa ufugaji wa nyuki kijiji cha Lulindi kata ya Ukwega baada ya kushambuliwa na nyuki Mwandishi Francis Godwin anaripoti toka Kilolo 

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 6 mchana baada ya mkuu huyo wa wilaya na msafara wake kutembelea mradi wa kijiji wa  ufugaji nyuki kwa ajili ya kukagua mradi huo wenye mizinga zaidi 92 .

nameagiza viongozi wa  serikali  za  vijiji vya kata ya Ukwega kuhamasisha wananchi kufunga nyuki na kulima kupanda Parachichi  kama mazao yao ya  kiuchumi 

Akizungumza wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kuhamasisha maendeleo katika vijiji vya Lulindi ,Ipalamwa ,Ukwega ,mkalanga na Makungu kata hiyo  ya Ukwega mkuu huyu alisema serikali haipendi kuona watu wake ni masikini wa kipato hivyo inapambana kuwawezesha kiuchumi zaidi .

Alisema Rais Dkt John Magufuli toka aingie madarakani amejipambanua kuwa ni Rais wa wanyonge na kazi kubwa anayoifanya ni kuona watanzania wote wananufaika na raslimali ya Taifa kupitia sera ya viwanda .

Kwani alisema ufugaji wa nyuki wenye tija na kilimo cha mazao ya biashara kama Parachichi na mazao mengine yatawezesha wananchi kukuza kipato chao .

Asia alisema viongozi wa serikali za vijiji hadi wao wa wilaya wanapaswa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi kuondokana na umasikini kama ambavyo kwa upande wake na viongozi wa wilaya hiyo wanavyofanya kuwafikia wananchi .

Kuhusu Kero ya maji kijijini hapo alisema atahakikisha anashirikiana na  viongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama .

Aidha alisema ili maendeleo yaweze kufanyika asingependa kuona kuna watu ambao hawafanyi kazi na kuagiza viongozi wa vijiji kuwabana wote wanaoshinda  vijiweni hasa vijana pia kuwawajibisha kisheria wanawake wanaokwenda kunywa pombe na watoto ama wale wenye ujauzito .

Pamoja na  kuagiza  kukamatwa kwa wanawake  hao watakaokutwa  katika maeneo ya  starehe usiku  pia  mkuu  huyo  wa wilaya ameagiza kukamatwa kwa  vijana  wote  wanaoshinda  vijiweni wakipiga  porojo  pasipo  kwenda  shamba kufanya  shughuli za  uzalishaji mali .

Alisema  haiwezekani viongozi wa  serikali  za  vijiji  kuendelea  kuwafumbia  macho  wanawake  wenye  tabia ya  kukaribisha udumavu kwa  watoto wao kwa  kuwanywesha  pombe  watoto    wadogo ama  kuona  wanawake  wajawazito  ambao kimsingi  wanatakiwa  kutunza mtoto  aliyepo  tumbuni  kwa  kula vyakula vinavyohitajika kwa  ajili ya afya ya  mtoto  aliyepo  tumboni  wakaachwa  wakinywa pombe usiku  kucha .


"Wewe  mwanamke  una  mtoto  mdogo ama  una ujauzito kwenye  pombe  usiku unatafuta  nini tena  nimeambiwa  kuwa wanawake  wanaokwenda wa watoto wachanga  kwenye  pombe  wakiona wana mambo yao ambayo yanazuia kwenda na mtoto wamekuwa  wakimnywesha  ulanzi ama pombe   kali mtoto  ili alale  usingizi na yeye  aendelee na starehe  zake  vichakani nasema  sitakubali kuona  watoto  wakihatarishiwa afya  zao kwa  kuendelea  kunyweshwa  pombe nasema kamateni  wote  na wapigeni faini ili faini  hizo  zifanye kazi  za  kimaendeleo katika   vijiji "  alisema Asia 


Kuwa hajazuia  wanawake hao  kunywa  pombe ila  amezuia  wanawake   wenye watoto na wajawazito  kukutwa kwenye pombe majira ya usiku na kama  wanatamani  pombe basi  ni  vizuri  wakanunua na kwenda  kunywa  nyumbani  wakati wakiwaandalia   watoto  chakula ila sio kugeuza  pombe na chakula kwa  watoto .


No comments:

Post a comment