Sunday, 22 December 2019

MBUNGE BONNAH AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA

Mbunge wa jimbo l Segerea Bonah Ladslaus akizungumza na wananchi wa Segerea wakati wa ziara yake .
Mbunge wa Segerea ,Bonah Ladslaus akiangalia maji mto Msimbazi Kata ya Segerea Manispaa ya Ilala

Picha na habari na Heri Shaaban

 MBUNGE wa Segerea  Bonnah Kamoli amewataka Wananchi wa jimbo la Segerea kushirikiana na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika kuleta Maendeleo Jimboni humo.

Bonnah aliyasema hayo Kata ya Segerea mtaa wa Segerea Manispaa ya Ilala Leo, alipokwenda katika ziara ya kutatua kero za wananchi.

" Wananchi wenzangu wa Jimbo la Segerea nawaomba tuwatumie Wenyeviti wetu vizuri Katika kuleta Maendeleo  ya mitaa yenu.

"Segerea tuna wenyeviti  wa Mitaa 61,  mkiwatumia vizuri  maendeleo yatakuja kwa kasi" alisema Mh.Bonnah .

Kamoli aliongeza kuwa Jimbo La Segerea lina Kata 13 Mitaa 61 na wakazi milioni 1.4. ni jimbo la kwanza kuwa na wakazi wengi nchini na pia Kata inayoongoza kwa kuwa na  wakazi wengi nchini Tanzania iko jimboni kwetu  kata ya Vingunguti.

Aliwataka  wananchi tukiwatumia wenyeviti vizuri kuwasilisha  taarifa za kero zao  ili ziweze kufika Ofisi ya Mbunge mapema pamoja na ofisi zingine za  serikali kwa ajili ya kuzitatua.

Alisema Jimbo hilo ni kubwa  linataka ushirikiano  katika kuleta Maendeleo.

Alisema katika jambo la maendeleo ushirikiano lazima   kuwasilishe  kero   serikali  za mitaa pamoja na kushiriki vikao vya kuleta Maendeleo.


 " Mimi kwa nafasi yangu nipo tayari kushirikiana na wenyeviti wote muda wote masaa yote 24 ,mmenichagua  ili niwatumikie".

Aidha katika ziara hiyo mbunge amehaidi kupeleka kifusi cha kokoto na mawe kwa ajili ya kuboresha miundombinu  ya eneo lililoharibiwa na maji ili kuweza kurudisha mawasiliano katika barabara ya mtaa wa Segerea na Migombani.

Wakati huo huo Mbunge Bonnah amewataka wakazi wa Mtaa wa Segerea ambao hawana Maji safi na Salama ya DAWASA kufika Ofisi ya serikali za mitaa kwa ajili ya kuorodhesha majina yao ili wapeleke maombi yao DAWASA ili waunganishwe Maji.


No comments:

Post a comment