Monday, 16 December 2019

MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA TANAPA NA NCCA KUPAMBA MOTO DISEMBA 23


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro yanatarajia kupamba moto katika viwanja vya Fort Coma nje ya Hifadhi ya Serengeti ambapo Wageni wa kitaifa na kimataifa watashiriki kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi enelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.


Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa Shirika Hifadhi za taifa (TANAPA) ,Dr.Allan Kijazi amesema kuwa hifadhi  ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi za Ngorongoro zilianzishwa kwa pamoja mwaka 1959 hivyo kwa pamoja zinasheherekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwake licha ya mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo zimepitia bado zimeweza kuingiza watalii wengi na kuliingizua taifa mapato makubwa.

Kijazi anasema kuwa maadhimishohayo yatapamwa na wageni kutoka nchi mbalimbali duniani,pamoja na watafiti wakubwa waliowahi kutafiti juu ya Hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro ,wadau wa uhifadhi ambao wamekua wakiunga mkono juhudi za uhifadhi watafika katika maadhimisho hao yatakayofanyika Disemba 23 mwaka huu .

Aidha amesema kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo anatarajia kuwa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh.Samia Suluhu  huku akiongozana na Viongozi wengine wa kitaifa ambao watashiriki katika maadhimisho hayo muhimu .

“Kabla ya Maadhimisho hayo kutakua na kongamano la uhifadhi litakalofanyika Disemba 21 mwaka huu katika eneo la  Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo litajumuisha wadau wa uhifadhi pamoja na Wataalamu wa masuala ya uhifadhi huku tukiangazia utalii endelevu kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla” Anaeleza Kijazi

Kwa upande wake Kaimu Kamishana  wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA),Asangye Bangu amesema kuwa Kongamano kubwa la uhifadhi litafanyika katika Mamlaka hiyo hivyo amewataka wadau kufika kwa wingi na kuhudhuria katika kongamano hilo muhimu kwa maendeleo ya uhifadhi.

Assangye amesema kuwa tayari Mamlaka hiyo imepata utambulisho wa utalii wa miamba na tayari wameanza kuingiza mapato kwa wingi suala ambalo litajadiliwa katika kongamano na namna ya kuongeza utalii.

Anasema kuwa pia kongamano hilo litaangalia namna ya kuboresha utalii wa mali kale ambao pia umekua ukiliingizia taifa fedha za kigeni.

No comments:

Post a comment