Mkuu wa wilaya Tabora mjini Ndg. Komanya Eric Kitwala tarehe 3 Disemba 2019 ameitisha kikao cha kazi kwa viongozi wa serikali ya Mtaa kutoka Mitaa 134, Vijiji 41 pamoja na Vitongoji  156 waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za Mtaa mwaka 2019 ikiwa ni pamoja na kuwapongeza.

Akiongea katika hadhara hiyo Ndg. Kitwala amewapongeza kwa kuchaguliwa kuongoza serikali ya Mtaa na kuwaasa kutumia dhamana hiyo kwa uadirifu na kuzingatia msingi wa utawala Bora, kanuni na miongozo ya matumizi ya fedha kwa weledi.

Mumebeba matarajio ya watanzania wengi ambao wana imani kubwa na uongozi wa awamu ya tano chini ya Jemedari  Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo zingatieni utumishi ulio karibu na wananchi kwa kutatua kero zao hususani upande wa ardhi  Ndg. Kitwala amesema.

Kwa nyakati tofauti Wenyeviti hao wamempongeza Mkuu wa Wilaya kuitisha kikao hicho chenye dhima ya kuwapongeza sanjari na maelekezo ya miongozo ya kazi. Hivyo wameahidi kuzingatia weledi wakati wa kutimiza majukumu yao.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo kimehudhuliwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Tabora Mjini Mhe. Mohammed Katete, Katibu Tawala Wilaya wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora

Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Tabora Mjini 🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: