Saturday, 28 December 2019

CCM MKOA WA MBEYA YATOA MSIMAMO KUHARIBIKA KWA UWANJA SOKOINE JIJINI MBEYATaarifa ya CCM Mkoa wa Mbeya, kuhusu tamasha la wasafi liliofanyika uwanja wa CCM Sokoine tarehe 25.12.2019. 


Baada ya Kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa wa Mbeya iliyokutana leo tarehe 27.12.2019. Mambo yafuatayo yaliambuliwa

Uwanja uliombwa na Mohamed Mashango kwa ajili ya tamasha la musiki tarehe 25.12.2019.

CCM Mkoa wa Mbeya ndio ilitoa idhini kwa Mohamedi Mashango kutumia uwanja wa Sokoine tarehe 25.12.2019 kwa barua ya tarehe 16.12.2019. ambayo ilimpa masharti ya matumizi ya uwanja, kuwa eneo la kuchezea mpira lisiguswe na mashabiki wa muziki. Na ikiwa utatokea uharibifu wowote atawajibika kutengeneza.

Mohamedi Mashango alikiuka masharti ya matumizi ya uwanja na kusabisha mashabiki wa muziki kuingia katika eneo la kuchezea mpira wa miguu na kufanya uharibifu mkubwa wa uwanja.

Kamati ya Siasa Mkoa wa Mbeya umemtaka Mohamedi Mashango afanye marekebisho ya uwanja ndani ya mwezi mmoja. Na Mohamedi Mashango amekubali kufanya ukarabati huo na ameishaanza kufanya ukarabati huo leo.

CCM Mkoa wa Mbeya inaviomba radhi vilabu vya mpira wa miguu vilivyokuwa vinautumia uwanja wa Sokoine kabla ya kufungiwa na bodi ya ligi kwa usumbufu na gharama wanazoingia kwa kutokutumia uwanja wa Sokoine. Vilabu hivyo ni Mbeya City, Tanzania Prison, Mbeya Kwanza, Boma FC, Ihefu FC na Tukuyu Star.

Mwisho tunawaomba radhi WanaCCM wote, wananchi na wapenzi wa michezo katika mkoa wa Mbeya kutokana na usumbufu mnaoupata kutokana na uharibifu uliotokea katika uwanja wa Sokoine na kusababisha uwanja huo kufungiwa na bodi ya ligi. CCM Mkoa wa Mbeya tunaendelea kufanya jitihada ili uwanja uweze kutengenezwa haraka na ufunguliwe na michezo kuendelea kuchezwa katika uwanja wa Sokoine
Imetolewa na

Bashiru S. Madodi
Katibu Siasa na Uenezi CCM
Mkoa Mbeya.

No comments:

Post a comment