Katibu mtendaji wa Baraza la kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt.Mwanahija Juma akizungumza na washiriki wa Kongamano la tatu la Kiswahili la Kimataifa lililofanyika Zanzibar

Na.Vero Ignatus,Zanzibar.

Baraza la kiswahili la Zanzibar (BAKIZA )imeandaa kanuni zitakazosimamia haki za waandishi kwa kukusanya mirabaha kutoka kwa taasisi za elimu mashirika ili kulinda kazi za waandishi.

Hayo yamebainishwa kwenye kongamano la tatu la kiswahili kwa siku mbili na kuwakutanisha washiriki 270 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Akizungumza Katibu mtendaji wa Baraza la kiswahili (BAKIZA) Dkt.Mwanahija Juma amesema kuwa washiriki wa kongamano la pili waliwashauri BAKITA na BAKIZA kuwaenzi waandishi wakongwe na kuhamasisha waandishi chipukizi kuandika kazi mbalimbali za kiswahili.

Amesema katika kuadhimisha siku ya kiswahili duniani kila mwaka wamekuwa wakihamasisha waandishi chipukizi kwa kuwafanyia mashindano na kuwapa mafunzo 

"Mwaka huu machi ,2019 walitoa mafunzo ya hadithi fupifupi kwa waandishi walioshiriki mashindano ya hadithi fupi"

Aidha walitoa azimio la kuwataka Bakiza litoe ithibati kwa vitabu vinavyochapishwa hivyo wametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wote wa vitabu wa zanzibar wasichapishe vitabu kabla ya kuvipitisha Bakiza ili kuvipa ithibati.

Amesema kuwa washiriki walitoa azimio la kuandaa ziara ya utalii wa Kifasihi jambo ambalo limefanyiwa kazi katika kongamano la tatu la mwaka 

"Tumeandaa ziara katika mitaa aliyoitaja mwandishi Shafi Adam Shafi katika kitabu cha Kuli iliwemo Bansatini ,Malindi,Darajani ,Msikitimabuluu,Gulioni,Kwahajitumbo,Kibiritingoma na Makaburimsafa.

Hivyo BAKIZA wameiomba Taasisi ya Hakimiliki iangalie upya mirabaha ya waandishi wa habari wanayopewa kutoka wauzaji wa vitabu na wachapishaji.

MWISHO.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: