Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.


Na. Aron Msigwa – WMU, ARUSHA.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) lifanye maboresho ya miundombinu ya huduma za dharula na uokoaji ndani ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro ili kuogeza usalama wa watalii wanaokweda 2kupanda mlima huo.

Pia, amelitaka shirika hilo liedelee kuboresha miudombinu ya malazi katika hifadhi hiyo ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa ya wapanda mlima na kuangalia uwezekano wa kutafuta wawekezaji watakaojenga hoteli za kisasa kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.

Dkt.Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati akipada mlima Kilimanjaro Septemba, 28 mwaka huu, akiwa ameambatana na kundi la Wasanii na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi.

Dkt. Kigwangalla ameieleza Menejimenti hiyo kuwa katika zoezi lake la kupanda mlima Kilimanjaro kuna changamoto alizibaini zikiwemo za kukosekana kwa miudombinu ya kutosha ya huduma za uokoaji na malazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuongeza ufanisi na idadi ya watalii wanaopanda mlima huo.

Kufuatia hali hiyo ameiagiza TANAPA ianze kuboresha huduma za dharula na uokoaji pia ijenge vituo vya kutolea tiba na huduma ya kwanza mlimani vitakavyokuwa na wataalam wa kuhudumia watalii wanaopata matatizo wakiwa mlimani pia kuboresha huduma za malazi katika baadhi njia za mlima huo.

Dkt.Kigwangalla amesema changamoto hizo zikitatuliwa kwa haraka zitauwezesha mlima huo kupata idadi kubwa ya watalii kuliko ilivyo sasa na kuiogezea serikali mapato.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za uokoaji (Rescue services) kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro ameiagiza TANAPA ifanye utaratibu wa kuazisha huduma ya viberege maalum (Zip line) vitakavyokua vinatumika kushusha wapada mlima watakaokua wakipata matatizo ya kiafya kwa haraka hata wakati wa hali mbaya ya hewa.

“Suala la matumizi ya “Zip line” mliongezee nguvu ya kulitekeleza, hii itakua njia rahisi ya uokoaji na itawajengea ujasiri wapada mlima waelewe kwamba hata kama watapata shida yoyote ya kiafya wakati wa kupanda mlima wanajua wana uhakika wa usalama wa maisha yao hata pale ambapo hali ya hewa ni mbaya na helikopta haiwezi kutua mlimani” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Amesema uwepo wa huduma hiyo ya kisasa ya kushusha watalii wanaopata chagamoto za kiafya itawezesha watalii kupata huduma mlimani kupitia vituo vya kutolea huduma ya kwanza vitakavyojegwa mlimani ambavyo vitakua na wataalam wenye mafumzo watakaokuwa na jukumu la kutoa huduma muda wote.

Kuhusu uboreshaji wa huduma ya malazi mlimani Dkt. Kigwangalla ameonesha kuridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na TANAPA kuboresha miundombinu ya malazi mlimani na kuitaka iangalie uwezekano wa kuhamasisha wawekezaji wakubwa kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa. 

Amesema uwepo wa hoteli hizo pamoja na mambo mengine utaongeza siku za watalii kukaa mlimani akitoa mfano wa hoteli nzuri na za kisasa zilizojengwa katika milima ya Alaps ambazo zinatembelewa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Kufuatia maagizo hayo, Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi amesema kuwa TANAPA inaendelea kufanya maboresho kwenye maeneo ya kulala wageni ili yaweze kwenda na wakati pia yawe na uwezo wa kupokea wageni wengi pia kuishirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma mlimani.

Amesema kazi ya kuainisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kisasa inaendelea na kwa kuanzia maeneo manne yamekwishaainishwa kwa ajili ya uwekezaji na kuongeza kuwa baadhi ya wawekezaji wamekwishajitokeza na kuonesha nia ya kujenga hoteli za kisasa katika mlima huo.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za ukoaji mlimani amesema kwa sasa kuna maeneo yana miundombinu ya barabara zinazowezwsha magari ya kubebea wagonjwa kufika katika baadhi ya maeneo na kutoa huduma ya uokoaji.

Pia amesema wamekua wakitumia helikopta kutoa huduma za uokoaji licha ya huduma hiyo kushindwa kufanyika kazi wakati wa hali mbaya ya hewa na hivyo kulazimika kutumia machela za matairi zinazoendeshwa na watu kuhudumia watalii wanaopata matatizo ya kiafya.

Aidha, Dkt. Kijazi amesema TANAPA inaendelea kufanya maboresho ya huduma za dharula na uokoaji na itawasilisha kwake taarifa ya utekelezaji itakayoainisha mpango wa ujenzi wa njia za kisasa zitakazotumia viberenge maalum vya uokoaji vitakavyokua vikipita kwenye waya (Zip line) ili kazi ya ujenzi wa njia hizo ianze mara moja. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: