Na Farida Saidy,Morogoro

Watu wasio julikana wamevamia na kuchoma moto Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mlali wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, na kuteketeza Nyaraka na baadhi ya samani, ambapo tayari watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi wakihusishwa na tukio hilo akiwemo diwani wa kata hiyo Frank Mwananjinje.

Tukio la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa ofisi hiyo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Novemba 11 ambapo nyaraka mbalimbali zimeteketea vibaya na baadhi ya samani ikiwemo Viti naMeza.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa kata hiyo ambae pia ni msimamizi wa uchaguzi, amesema hivi karibuni alipokea vitisho kutoka kwa mmoja wa wagombea akimtuhumu kuto tenda haki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata hivyo Tukio hili limeifikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa kushuhudia madhara yaliyo tokea, ambapo mkuu wa mkoa huu Loata Ole Sanare anasema kilicho fanyika ni uvunjifuwa amani,sambamba na kulitaka jeshi la polisi kuwasaka wahusika.

Pamoja na mambo mengine kufuatia tukio hilo mkuu wa mkoa amewataka wakuu wa wilaya zote kushirikiana na vyombo vya usalama, kuweka ulinzi wa kutosha katika ofisi zote za serikali katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: