Saturday, 23 November 2019

Wasimamizi Wa Uchaguzi Wa Vituo Vya Kupiga Kura Waaswa Kuwa Waadilifu

Msimamizi wa  Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba Ahmada Suleiman amewaomba wasimamizi katika vituo vya kupiga kura kuwa waadilifu sambamba na kuwahi katika maeneo yao ya vituo siku ya uchaguzi jpili

Akizungumza kwenye semina  na wasimamizi wa vituo wa Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji mwaka 2019, alisema kuwa wafanye kazi hiyo katika weledi na uaminifu ili zoezi liishe katika amani na utulivu

" Sisi ni miongoni mwa Wilaya ambazo tunafanya uchaguzi hivyo ninyi wasimamizi hakikisheni  wananchi wanatimiza haki yao bila vikwazo vyovyote visivyo vya lazima," alisema Ahmada

Naye mwezeshaji George Kashura aliwaeleza kuwa wanatakiwa kufuata taratibu za kufungua kituo na kufunga "Mkifika kwenye vituo vyenu hakikisheni mnaweka  vifaa vyenu sawa ili muweze kwenda na muda unatakiwa," alisema Kashura.

Uchaguzi katika Wilaya ya Tandahimba unatarajiwa kufanyika jpili katika Kata ya Tandahimba na Kata ya Nanhnyanga.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba akizungumza na wasimamizi wa vituo vya kumpigia kura.

 Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya kumpigia kura
 Mmoja Kati ya wasimamizi wa kituo akionyesha jinsi ya kufunga sanduku la kura
 Mwezeshaji George Kashura akiwapa maelekezo wasimamizi wa vituo

No comments:

Post a comment